Mbunge
wa Mbeya kupitia CHADEMA Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, amesema
alishangazwa na kitendo cha kusikia imepigwa simu kutoka juu, na kueleza kwamba
ni lazima yeye na Masonga wavae sare za jela
Akizungumzia suala hilo Sugu amesema
kwamba kitendo hicho kilimshangaza kwani kulikuwa kuna watu wengine wengi
walikuwa hawana sare na wamefungwa mule muda mrefu lakini walikosa sare, hivyo
kitendo cha kulazimishwa yeye ambaye yuko kwa muda mfupi kilikuwa
kinamshangaza.
“ Nisiite kujisikia vibaya niite
kushangaa, ni siku ambayo maagizo kutoka juu, ilipigwa simu kwamba lazima Sugu
avae uniform na Masonga, unaweza ukaona kwamba zaidi ya wafungwa 600 hawana
uniform, Sugu yuko pale mmemfunga kwa miezi mitano, anatakiwa kutumikia kama
miezi mitatu, lakini unamlazimisha avae uniform, lakini kuna wafungwa pale
wamefungwa maisha mamia kwa mamia hawana uniform, kwa nini usiangalie namna ya
kuwapatia wale uniform unahangaika na mtu ambaye anapita tu!?”, amesema Sugu.
Sugu ameendelea kwa kusema kwamba
kitendo cha yeye kulazimishwa kuvaa sare hakikumkwaza kwani aliona inamsaidia
kuhifadhi nguo zake.
“Zilitafutwa siku hiyo hiyo uniform,
wakaja wakatuletea uniform ambazo zimevaliwa tukagoma, tukakataa kwa sababu
hatuwezi kuvaa nguo ambazo hatujui zimevaliwa na nani, wakaenda kuhangaika kila
kona sijui walitoa Segerea, lakini walitumia nguvu kuhakikisha wanatuvalisha
uniform, wao walidhani wakimvalisha Sugu uniform ataathirika kisaikolojia,
lakini we umeshanifunga kuvaa nguo ni kitu gani, kwanza utanisaidia kutunza
nguo zangu", amesema Sugu.
Sugu aliachiwa huru mapema wiki
iliyopita kwa msamaha wa Rais baada ya kutumikia kwa muda mfupi kifungo chake
cha miezi mitano katika gereza la Ruanda mkoani Mbeya, akiwa na mwenzake
Emmanuel Masonga
No comments:
Post a Comment