HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday 30 November 2014

HII NDIO HISTORIA YA MWANAHARAKATI WA KWELI **Che Guevara**






Mwanaume huyo aliyekuwa na wajihi wa kuvutia alikuwa raia wa Argentina aliyezaliwa Juni 14, 1928 na akafariki Oktoba 9, 1967 huko Bolivia alikouawa akiendesha mapambano dhidi ya manyanyaso ya watawala.
Umaarufu wa Che Guevara (hutamkwa Che Gevara) ulijitokeza sana duniani alipoungana na wapiganaji wa Cuba waliokuwa wamekimbilia Argentina ili kupanga mapambano dhidi ya utawala wa Fulgencio Batista wa Cuba.
Che – jina maarufu ambalo kwa Kihispania ni “kakitu” --aliungana na kina Castro na kwenda nao Cuba kuendesha mapambano na kuuangusha utawala wa Basitsta mwaka 1959 ambapo baadaye akawa waziri wa viwanda.



Hata hivyo, baadaye aliuacha wadhifa huo na “kutokomea” kwengine ambako aliendeleza mapambano dhidi ya watawala wa kidikteta duniani.
Katika mapambano hayo hakusita kuwachochea watu wasikubali kuwekwa mifukoni na watawala ambao wakishika madaraka au kufika ikulu huwafanya watu wengine wapumbavu.

Mwaka 1967 alifika nchini Tanzania wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere na akajiunga na wapiganaji wa Congo waliokuwa wakiendeleza mapambano dhidi ya utawala wa aliyekuwa dikteta wa nchi hiyo, Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga.
Wapiganaji hao walikuwa ni pamoja na aliyekuja kuwa Rais wa Congo, Laurent Kabila, baba wa rais wa sasa wa nchi hiyo, Joseph Kabila ambaye alikulia na kusomea Tanzania shule ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, makazi yao yakiwa Kunduchi.
Ni Ernesto Che Guevara ambaye watu wengi huvaa T-shirt za picha yake na kuweka ‘stickers’ kibao kwenye magari na sehemu mbalimbali bila kumfahamu picha yake ni maarufu zaidi duniani.
Karl Max
Kwa kifupi picha yake hiyo ilipigwa na Alberto Koda kwenye mazishi huko Havana siku ya kuomboleza watu waliokufa katika meli ya La Coubre iliyotegwa bomu na majasusi wa Marekani na kuua watu Wengi.

*MUHIMU*** Ernesto Rafael Guevara de la Serna au Che Guevara alikuwa mtabibu mzaliwa wa Argentina aliyekuwa mfuasi wa itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx. Guevara anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na Afrika.

Wakati akisomea utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Marekani ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe umasikini uliokithiri. Alisikitishwa sana na maisha ya ufukara waliokuwa wakiishi wananchi wengi huku wachache wakiwa wanamiliki mali za nchi hizo. Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili hali hii na kuamua kuwa njia pekee ya kuondoa umasikini na ukandamizaji ni mapinduzi. Aliamua kusoma kwa undani falsafa za Karl Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati za kisoshalisti nchini Guatemala chini ya rais Jacobo Arbenzi Guzmán.
Fidel Castro

Mwisho mwa miaka ya 1950, Guevara aliungana na Fidel Castro aliyekuwa akiongoza kundi la kijeshi lililotwaa madaraka kwa nguvu nchini Kuba mwaka 1959. Guevara alikuwa mmoja wa viongozi wa serikali mpya ya Kuba. Katika kipindi hiki, Guevara aliandika vitabu na makala mbalimbali kuhusu nadharia na vitendo vya vita vya msituni kwa nia ya kuondoa madarakani tawala za kibepari na kibeberu.

 Guevara aliondoka nchini Congo na kuelekea Bolivia ambapo alikamatwa mwaka 1967 na jeshi la Bolivia likishirikiana na majasusi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA). Baada ya kukamatwa kwake aliuawa kinyama.
Baada ya kifo chake, Guevara alichukuliwa kama nguzo ya vuguvugu la kimapinduzi ya kishoshalisti duniani. Picha yake na kofia aina ya Beret aliyopenda kuivaa vimekuwa kama alama za mapinduzi ya mrengo wa kushoto duniani.
 Watu wengi wengi huvaa T-shirts zenye picha yake bila kujua alikuwa ni mpiganaji wa kimataifa aliyepigania haki za wanadamu wenzake duniani badala ya kuleweshwa na madai ya amani na utulivu yanayosemwa kwa ulaghai na viongozi wengi wanafiki duniani.

No comments:

Post a Comment