Alvaro Morata |
MSHAMBULIAJI
nyota wa klabu ya Real Madrid, Alvaro Morata amefanikiwa kukamilisha uhamisho
wake kwenda Juventus kwa ada ya euro milioni 20.
Morata
aliwasili jijini Turin jana kwa ajili ya vipimo vya afya kwa mabingwa hao wa
italia baada ya kupita wiki kadhaa ya tetesi juu ya uhamisho huo. Juventus sasa
wamethibtisha kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa mkataba wa miaka
mitano.
Katika
makubaliano ya mauzo ya mchezo huyo, Madrid watapewa kipaumbele cha kuuziwa
mchezaji huyo katika misimu miwili ijayo kama wakimhitaji tena kwa ada ambayo
haitazidi paundi milioni 30.
Fabio Borini |
KLABU
ya Liverpool imekubalia kumuuza mshambuliaji wake Fabio Borini kwenda klabu ya
Sunderland kwa ada ya paundi milioni 14. Borini mwenye umri wa miaka 23 alikuwa
akicheza kwa mkopo katika klabu hiyo msimu uliopita na kuisaidia isishuke
daraja.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Italia alifunga mabao 10 akiwa na Sunderland na kupelekea
kuibuka na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka anayechipukia. Borini ambaye alikuwa
mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Brendan Rodgers wakati akitua Liverpool,
alihamia Anfield akitokea Roma kwa ada ya paundi milioni 11 Julai mwaka 2012.
Hata
hivyo, mshambuliaji huyo kiwango chake kiliyumba toka alipotua Liverpool na
kufunga mabao mawili katika msimu wa 2012-2013 kabla ya kupelekwa kwa mkopo
Sunderland.
MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho |
MENEJA
wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema usajili wake katika kipindi hiki cha
majira ya kiangazi umekamilika kufuatia kumsajili beki wa kushoto Filipe Luis
kutoka klabu ya Atletico Madrid. Luis anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na
Chelsea baada ya viungo Cesc Fabregas na Mario Pasalic pamoja na mshambuliaji
Diego Costa.
Akihojiwa
Mourinho amesema wamemaliza usajili jana wakati muda rasmi wa kumalizika kwa
usajili ni Agosti 31 na kuishukuru klabu yake kwa kazi nzuri sio kwasababu ya
wachezaji walionunua bali kuweka rekodi kwa kusajili kwa muda mfupi.
Chelsea
wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kuwataka wachezaji mbalimbali ghali katika
kipindi hiki cha kiangazi akiwemo nyota wa Real Madrid na Ujerumani Sami
Khedira na mshambuliaji wa Monaco radamel falcao. Hata hivyo Mourinho
amesisitiza kuwa ameridhishwa na bishara waliyofanya klabu yake katika kipindi
hiki kwani tayari wameshapata wachezaji wote waliowahitaji.
Frank Lampard |
KIUNGO
mkongwe wa zamani wa Uingereza, Frank Lampard anatarajia kumamilisha usajili
katika klabu mpya ya Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS ya New York City wiki
ijayo.
Klabu
hiyo ilifanikiwa kumshawishi nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 baada ya
mkataba wake na Chelsea kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.
Kwasasa
lampard yuko katika likizo fupi baada ya kuitumikia timu ya taifa ya Uingereza
katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil. Hata hivyo
kiungo huyo anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu mpya wa MLS
mwaka 2015.
LIVERPOOL YAMNUNUA LOIC REMY
WA QPR
Loic Remy |
LIVERPOOL
imeripotiwa kufanya ununuzi wake wa 5 kabla Msimu mpya kuanza kwa kumnunua
Straika wa QPR Loic Remy.
Remy,
Mchezaji wa Kimataifa wa France mwenye Miaka 27, Msimu uliopita alikuwa kwa
Mkopo huko Newcastle na kufunga Bao 14 katika Mechi 26 za Ligi Kuu England.
QPR
wanalazimika kupokea Pauni Milioni 8.5 na kumruhusu Mchezaji huyo aondoke kama
Mkataba wake unavyotaka ikiwa Dau hilo litafikiwa.
Awali
ilidhaniwa Arsenal watamchukua Mchezaji huyo ambae ameichezea France Mechi 27
na kufunga Bao 5 lakini sasa inelekea Liverpool wamechukua hatua za haraka
kukamilisha Uhamisho wake.
Liverpool,
chini ya Meneja wao Brendan Rodgers, tayari wameshanunua Wachezaji wanne kwa
ajili ya Msimu mpya ambao ni Adam Lallana, Rickie Lambert, Emre Can na Lazar
Markovic.
Kutua
kwa Remy Liverpool kutaifanya safu yao ya mashambulizi kuwa mpya ikiwajumuisha
Ricky Lambert na Daniel Sturridge baada ya kuwapoteza Luis Suarez alieuzwa
Barcelona, Iago Aspas aliepelekwa kwa Mkopo huko Sevilla na Fabio Borini
alienunuliwa na Sunderland.
BPL-LIGI
KUU ENGLAND
RATIBA
MECHI ZA UFUNGUZI
**Saa
za Bongo
Jumamosi
Agosti 16
14:45
Man Utd v Swansea [Old
Trafford]
17:00
Leicester v Everton
[King Power Stadium]
17:00
QPR v Hull [Loftus Road
Stadium]
17:00
Stoke v Aston Villa
[Britannia Stadium]
17:00
West Brom v Sunderland
[The Hawthorns]
17:00
West Ham v Spurs [Boleyn
Ground]
19:30
Arsenal v Crystal Palace
[Emirates Stadium]
Jumapili
Agosti 17
15:30
Liverpool v Southampton
[Anfield]
18:00
Newcastle v Man City
[St. James' Park]
Jumatatu
Agosti 18
22:00
Burnley v Chelsea [Turf
Moor]
No comments:
Post a Comment