Watendaji
mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mabwana na Mabibi afya wametakiwa kusimamia
suala la usafi wa mazingira kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo
ya viwandani.
Akitoa majumuisho ya ziara ya Kamati ya Uchumi Elimu na Afya ya Halmashauri ya
jiji la Tanga, Mwenyekiti wa kamati hiyo Seleboss Mustafa, amesema hali ya
usafi katika viwanda jijini hapa ni mbaya na inahatarisha maisha ya wafanyakazi
na wananchi waishio karibu na maeneo husikaHayo yamejiri mara baada ya kamati
hiyo inayoundwa na wajumbe ambao ni madiwani kufanya ziara ya kustukiza katika
viwanda mbali mbali jijini hapa na kukuta hali ya wafanyakazi na usafi wa
mazingira si ya kuridhisha.
Aidha kamati
hiyo imetoa maagizo kwa watendaji wa Idara kuhakikisha ada ya ulipaji wa taka
ngumu,na malipo ya kodi mbalimbali yanalipwa kwa wakati.
Ziara hiyo
ya kamati ya uchumi elimu na afya imefanywa kwa siku moja ikiwa na lengo la
kuangalia usafi, huduma za afya kwa wafanyakazi, na ulipaji wa ada mbalimbali
katika halmashauri ya jiji la Tanga.
 |
|
 |
Mgodi wa malighafi za
kuzalisha saruji ( limestone) ulioko kwenye kiwanda cha Tanga Cement ambao
umekuwa ukitoa malighafi hizo tangu kuanzishwa kwa Kiwanda hicho miaka zaidi ya
30 iliyopita.
|
No comments:
Post a Comment