Na Masanja Mabula PEMBA
Watu
19 wakaazi wa shehia ya Sizini Tumbe Wilaya ya Micheweni wamelazwa
katika hospitali ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakipatiwa
matibabu baada ya kula samaki aina ya pono na puju wanao daiwa kuwa na sumu.
SAMAKI
BUNJU
|
Tukio
hilo limetokea siku ya jumatano ya tarehe 23 mwezi huu majira ya saa
12:30 za jioni katika Shehia ya Sizini baaa ya watu hao wa ukoo
mmja kutumia samaki wakati wa kula futari na kupelekea hali zao
kuanza kubadilika .
Baadhi
ya ndugu wa jamaa waliolazwa hospitalini wamesema kuwa hali za ndugu zao
zilianza kubadilika usiku majira ya saa saba na hivyo kuamua kuwakimbiza
hospital kwa ajili ya kupata matibabu kunusuru hali zao.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kaskazini Pemba
Sheikhani Muhammedi Sheikhani amethibitisha kutokea kwa tokeo hilo na kusema
kuwa waathirika wa tukio hilo wanaendelea na matibabu katika hospitalini hapo.
Aidha
shekhan ametowa wito kwa jamii na kuitaka kuwa makini wakati wanapotumia samaki
hasa wanaodaiwa kuwa na sumu ili kuweza kulinda maisha yao .
Kufuatia
kutokea kwa tokeo hilo mbunge wa jimbo la Tumbe Rashid Ali abdallah amelezea
kusikitishwa na kuwataka wananchi wawe na uvumilivu katika kipindi
hichi na kuwataka madaktari kuongeza juhudi za kazi ili kusaidia kuokoa maisha
ya watu hao .
No comments:
Post a Comment