RANIERI SASA KUWA KOCHA WA
UGIRIKI.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62
amesaini mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Fernando Santos
aliyekiongoza kikosi cha timu hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia mpaka
hatua ya mtoano alipongolewa na Costa Rica kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Ranieri ambaye aliiwezesha klabu ya
Monaco ambayo ilikuwa imepanda daraja katika Ligi Kuu nchini Ufaransa kumaliza
katika nafasi ya pili msimu uliopita lakini amekuwa akishukutumiwa vikali hatua
mabayo imepelekea kuangalia nafasi nyingine.
Kibarua cha kwanza cha Ranieri
akiifundisha Ugiriki itakuwa ni kuhakikisha wanaanza vyema mechi zao za kufuzu
michuano ya Ulaya mwaka 2016, ambapo Septemba 7 mwaka huu watakwaana na
Romania.
Ugiriki ambao walinyakuwa taji la
michuano hiyo miaka 10 iliyopita pia watachuana na Hungary, Finland, Ireland
Kaskazini na Visiwa vya Faroe katika kundi F walilopangwa.
DIDIER DROGBA ARUDI TENA CHELSEA CHINI YA MOURINHO!
Didier
Drogba amerudi Chelsea kama Mchezaji huru na kusaini Mkataba wa Mwaka mmoja.
Drogba,
mwenye Miaka 36, alitwaa Vikombe 10 alipokuwa Chelsea kati ya Miaka 2004 na
2012.
Mwaka
2012 aliondoka Chelsea na kwenda kujiunga na Klabu ya China Shanghai Shenhua
kisha kujiunga na Galatasaray Januari 2013 na kufunga Bao 5 katika Mechi 13
wakati Klabu hiyo inatwaa Ubingwa wa Uturuki.
Msimu
uliofuata aliifungia Galatasaray Bao 10 katika Mechi 32 na pia kuifikisha Robo
Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo walifungwa na Chelsea.
Akiongelea
kurudi kwake Chelsea, Drogba amesema: “Ulikuwa ni uamuzi rahisi. Siwezi kukataa
kufanya kazi na Mourinho!”
Nae
Meneja wa Chelsea, Jose Mouriho amesema Straika huyo mkongwe kutoka Ivory Coast
ni ’Mtu wa Chelsea.’
BEBE AJIUNGA
BENFICA YA URENO!
Benfica
wamehibitisha kumsaini Mchezaji wa Manchester United Bebe kwa Mktaba wa Miaka
Minne.
Bebe
alijiunga Man United kutoka Klabu ya Ureno Guimaraes Mwaka 2010 kwa Dau la
Pauni Milioni 7.4 lakini alikuwa hana Namba ya kudumu na alicheza Mechi kubwa 2
tu, Kombe la Ligi mara 2 na UEFA CHAMPIONZ LIGI Mechi 1 tu.
Man
United imethibitisha Uhamisho huu na imepata Dau la Pauni Milioni 2.4 na
itapata Asilimia 50 ya Mauzo yake yoyote ya baadae.
BEKI CALUM CHAMBERS ATUA ARSENAL..!
Beki
wa Southampton Calum Chambers amesaini kuchezea Arsenal kwa Dau la Pauni
Milioni 16.
Jana
Mchezaji huyo mwenye Miaka 19 anaechezea Timu ya Vijana ya England ya chini ya
Miaka 19 alifanyiwa upimwaji afya yake.
Chambers
anakuwa Mchezaji wa Tatu kusainiwa na Arsenal baada ya pia kuwanasa Fowadi wa
Barcelona Alexis Sanchez na Beki wa Newcastle Mathieu Debuchy.
Hadi
sasa Southampton imeshawapoteza Rickie Lambert na Adam Lallana waliokwenda
Liverpool na Luke Shaw aliekwenda Man United.
DEJAN LOVREN SASA KUPIMWA AFYA
LIVERPOOL
Beki wa Southampton Dejan Lovren
atapimwa afya Liverpool ili kukamilisha Uhamisho wake wa Pauni Milioni 20.
Beki huyo mwenye Miaka 25 kutoka
Croatia aliichezea Nchi yake Mechi zote 3 za Kombe la Dunia huko Brazil.
Hadi sasa Liverpool imesaini Wachezaji
wapya Wanne kwa ajili ya Msimu mpya ambao ni Rickie Lambert na Adam Lallana
kutoka Southampton, Emre Can kutoka Bayer Leverkusen na Lazar Markovic toka
Benfica.
ASAMOAH GYAN AONGEZA
MKATABA NA AL AIN.
NAHODHA wa timu ya taifa ya
Ghana, Asamoah Gyan ameongeza mkataba wake na klabu ya Al Ain ya Falme za
Kiarabu ambao unamalizika mwaka 2018.
Mshambuliaji huyo wa zamani
wa Sunderland alikuwa amebakisha mkataba wa miaka mwili na nusu lakini
aliongezwa mkataba mwingine ulioboreshwa zaidi jana.
Gyan mwenye umri wa miaka 28
amekuwa mfungaji anayeongoza katika Ligi Kuu ya huko kwa kipindi cha miaka
mitatu mfululizo. Nyota huyo ambaye alijunga na Al Ain akitokea Sunderland
kwa mkopo mwaka 2011, amefunga mabao 82 katika mechi 66 za ligi alizocheza.
No comments:
Post a Comment