HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday 27 January 2015

MAGAIDI WA ALSHABAAB NA ALQAEDA WAVAMIA TANGA "WAJERUHI NA KUPORA BUNDUKI KWA ASKARI POLISI WA DORIA USIKU"



Konstebo Mansur ambaye amelazwa katika hospitali ya Bombo baada ya kuchomwa kisu sehemu mgongoni na shingoni wakati wa uporaji huo
Majambazi yanayohusishwa na mtandao wa kigaidi wa Alqaeda pamoja na kundi la Alshabaab, wamewajeruhi askari polisi na kuwapora bunduki mbili aina ya Sub-Machine Gun (SMG) zilizokuwa na risasi 60 jijini Tanga.

Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jan 27 na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Tanga, Juma Ndaki, ambapo amesema tukio hilo limetokea katikati ya mitaa ya barabara ya 4 na 5 Jijini Tanga,  nyumbani kwa Jamali Twalib mwenye biashara ya kuuza chips Jijini hapa.

Polisi walioporwa bunduki hizo ni mwenye namba H 507 Konstebo Mwalimu na mwenzake G 369 Konstebo Mansur ambaye amelazwa katika hospitali ya Bombo baada ya kuchomwa kisu sehemu mgongoni na shingoni wakati wa uporaji huo na hali yake bado tete katika hospitali hiyo.

Mmoja ya mashuhuda wa tukio hilo, kijana muuza Chips Jeirus Chimya, amebainisha kuwa tukio hilo lilitokea majira ya 5:45 usiku wakati askari hao waliokuwa na kawaida ya kula hapo wanapokuwa doria usiku, walifika kwa ajili ya kupata mlo wa usiku.

"Kawaida askari hawa huwa wanafika wakiwa wanne na pikipiki zao na kula chakula hapa kila siku, sasa jana walifika wawili wakasema wenzao wamewaacha kituo cha basi cha Ratco watakuja wawawekee nao chakula chao, tukawaandalia kama kawaida," alisema Chimya.

Alisema baada ya kuwaandalia chakula kile ghafla waliwaona watu wanne wakiwafuata huku mmoja akiwa amebaki kwenye kona ya barabara ya 5 kutazama watu huku akiwa na pikipiki mbili ambazo walifika nazo kwenye tukuio hilo.

Chimya alisema askari wale walikuwa pembeni ng'ambo ya barabara kwenye duka moja linalouza nguo, wakikaa peke yao ndipo mmoja wa jambazi huyo alikuwa amevaa suruali wanayovaa askari wa Kutuliza ghasia FFU na kumvamia Mansur ambaye kwa wakati huo alikuwa akinywa soda.

"Yule jambazi aliyeonekana kama askari polisi alipoishika ile bunduki ya Mansur ambaye alitaharuki na jambazi kutoa kisu kwa lengo la kukata mkanda wa bunduki ili aondoke nayo akamchoma kisu cha shingo, lakini askari akawa mbishi akachomwa kisu kingine cha mgongoni akaiachia bunduki," alisema muuza chips huyo.

Aliendelea kueleza kwamba majambazi wengine wawili walimshika Mwalimu naye na kumpora bunduki yake na baada ya kuleta ubishi walimpiga na kisha kuangukia kwenye mtaro na kuichukua bunduki ile kirahisi na kukimbia katika eneo hilo.

"Kukweli watu tulioshuhudia tulipigwa na bumbuwazi tukizani ni utani baina ya askari kwa askari kutokana na namna walivyokuwa wamevalia watu wale kwani baada ya kupora bunduki hizo mmoja wa majambazi alishindwa kukimbia baada ya kupoteza funguo ya pikipiki.

Alisema baada ya muda askari wengine wawili waliokuwa wamewawekea chakula walifika katika eneo hilo huku majambazi wale wakiwa tayari wameondoka lakini wakafanikiwa kumkamata jambazi mmoja ambaye alikuwa akishindwa kuwasha pikpiki kutokana na kupoteza funguo.

Akizungumza ofisi kwake tukio hilo, kaimu kamanda wa polisi JUma Ndaki, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba mmoja wa majambazi waliomkamata na kumpekua nyumbani kwake walimkuta na CD zipatazo 13 zikiwa na mafunzo ya Alqaeda na Alshabaab.

"Ni kweli askari wetu wamenyany'anywa bunduki zikiwa na risasi 60 na mmoja wao tumemkamata na tulipompekua alikuwa na CD zenye kuonyesha mafunzo ya Alqueda bila shaka ni washirika wa kundi hilo na hivi sasa tunafanya mipango tumsafishe Jijini Dar es salaam kwa hatua zaidi za kiuchunguzi," alisema Ndaki.

Ndaki pia alisema walimkamata mmoja wa mke wa jambazi aliyemtaja kwa jina moja la Asha ambaye aliwahi kukamatwa kisha kuachiwa kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa Alqueda na kwamba kwa sasa mumewe ni mmoja kati ya waporaji wa bunduki hizo.

No comments:

Post a Comment