Mstahiki Meya wa jiji la Tanga, Omar Guledi |
Na Mwandishi Wetu.TANGA
Mstahiki
Meya wa jiji la Tanga, Omar Guledi,
ametoa agizo kwa mabalozi wa nyumba kumi
na wenyeviti wa Serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi kuweka mazingira ya
usafi maeneo yao na atakaekaidi achukuliwe hatua za kisheria.
Meya
Guledi ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa utunzaji na uhifadhi wa
mazingira kwa kata ya Nguvumali na kushirikisha viongozi wa kata, Serikali za
mitaa na viongozi wa dini ambapo amesema magonjwa ya milipuko na homa za mara
kwa mara hazitoisha hadi jamii yenyewe itakapobadilika juu ya usafi wa mazingira na usalama wa Afya zao.
Amesema
kufuatia kukaribia kwa msimu wa mvua ni wajibu wa kila kaya kuweka mazingira ya
usafi katika maeneo yao ikiwa na pamoja na kuifanyia usafi mifereji iliyoziba
ili kuwa rahisi mvua inaponyesha maji kutembea.
Naye
Katibu wa Asasi ya Nguvumali Commity Development of Enviromment (NCDE), Frank
Mgunda, amesema kumeongezeka vitendo vya uharibifu wa mazingira hivyo asasi
hiyo itafanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kutoa elimu ya mazingira kwa kuanzia
mjini hadi vijijini kabla ya msimu wa mvua kuanza.
No comments:
Post a Comment