Mkuu wa
Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subila Mgalu
|
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya
Muheza mkoani Tanga, Subila Mgalu, ameahidi kusimamia upimaji ardhi wa shamba
la mkonge Kibaranga ili wananchi wapate ardhi ya kulima.
Alitoa ahadi hiyohivi
karibuni wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika
Kibaranga, baada ya kutokea mgogoro kati ya wananchi na maafisa ardhi
waliyopewa kazi ya kupima shamba hilo.
Alisema kuwa kazi ya
kupima shamba hilo imeanza lakini kuna baadhi ya watu wanaendeleza mgogoro kati
ya wananchi na serikali.
Hatua hiyo inafuatia
maafisa ardhi wilaya ya Muheza kuanza kupima shamba hilo ili wananchi wapatiwe
maeneo ya kilimo.
Alisema kuwa baadhi
ya watu wanadanganya wananchi hao kuwa tayari maafisa ardhi wanagawa
mashamba kwa kupewa kitu kidogo, kitu ambacho si cha kweli. Alisema
amesikitishwa na kitendo cha wananchi hao kufukuza maafisa ardhi kwa
kutumia mapanga wakati mchakato huo ukiwa unaendelea vizuri baada ya agizo la
Rais Jakaya Kikwete la kukubali shamba hilo wapewe wananchi.
Alisema kuwa kwa sasa
wanafanyakazi hiyo ya upimaji kwa shida kwani inatakiwa zaidi ya Sh. Milioni
100 lakini wanapima kwa Shilingi Milioni nane tu ambazo wamepewa na wafadhili
kufanya kazi hiyo.
Mgalu alisema kuwa
yupo tayari kufa ili kuhakikisha shamba hilo linapimwa ili wananchi wapewe
ardhi hiyo.
Aliwataka wananchi
kuwa wavumilivu ili zoezi hilo liende vizuri ili wananchi wapate ardhi.
Kwa upande wake Afisa
ardhi ambae alikuwa anaendesha zoezi la upimaji shamba hilo, Daniel Mkwizu,
alisema kuwa zoezi lilikuwa linaendelea vizuri lakini wananchi waliwafukuza
na mapanga na kulisitisha.
No comments:
Post a Comment