Mshambuliaji wa klabu ya League 1 ya nchini Ufaransa ya Bastia Brandao
amepewa adhabu ya kifungo cha mwezi mmoja jela kufuatia kumtwanga kichwa kiungo
wa klabu ya PSG, Thiago Motta, tukio lilotokea kwenye mchezo wa ligi hiyo.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa, tayari amekwishakutana na
adhabu nyingine, akipewa rungu la kuwa nje ya kabumbu kwa kipindi cha miezi
sita kutokana na tukio hilo, kwenye mchezo ambao PSG iliibuka na ushindi wa
mabao mawili kwa sifuri mnamo August 16.
Bastia Brandao(kushoto) |
Kwa upande wake Motta, mwenye umri wa miaka 32, aliachwa akivunjika pua
kutokana na tukio hilo la kushambuliaji na Brandao, ambae pia alitozwa faini ya
pauni 15,850 ambazo ni sawa na Euro 20,000.
Hata hivyo, mwanasheria wa Brandao anasema alitarajia mshambuliaji huyo
angepewa adhabu ya kuitumikia jamii, na si kuwekwa jela.
Thiago Motta |
Brandao,ambae alishinda taji la ligi ya Ufaransa akiwa na klabu ya
Olympique de Marseille msimu wa mwaka 2010, ametamka kwamba kiungo Motta
alimtolea maneno ya kibaguzi ndani ya mchezo.
Kwa mujibu wa Motta akitoa ushahidi wake kwa polisi amesema kwamba,
wakati Brandao akifanyiwa mabadiliko, alimwambia kuwa atamsubiri kwenye Korido
lakini yeye hakutilia maanani, na ndipo alipomkuta na kukumbana na kadhia hiyo,
akinaswa na kamera.
Nae raisi wa klabu ya PSG Nasser Al-Khelaifi akitoa maoni yake amesma
kwamba, mshambuliaji Brandao alipaswa kufungiwa maisha kutokana na kitendo
chake alichofanya.
Hii na ile ya Zizzou ni tofauti???
No comments:
Post a Comment