Mahakama
ya Hakimu Mkazi Morogoro imeahirisha kesi ya tuhuma za kuchoma ofisi ya
Serikali ya Kijiji cha Sofi baada ya mshtakiwa wa kwanza, Suzan Kiwanga kuugua
ghafla.
Kabla ya kuhairishwa kwa kesi hiyo
leo Alhamisi Mei 17, 2018, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa
Serikali, Sunday Hyera ulionekana kutokubaliana na taarifa hizo za
ugonjwa.
Hali hiyo ilimfanya hakimu
anayesikiliza kesi hiyo, Ivan Msack kumtaka mdhamini pamoja na wakili wa upande
wa utetezi, Barthelomew Tarimo kuwasilisha taarifa ya daktari itakayothibitisha
taarifa hizo za ugonjwa.
Wakili Tarimo na mdhamini wa Kiwanga
walitoka na kwenda kuchukua taarifa hiyo ya daktari wa kituo cha afya cha Aga
khan iliyoeleza kuwa Kiwanga anasumbuliwa na kichwa na maumivu ya mwili na
kuiwasilisha mahakamani.
Katika taarifa hiyo ya daktari
ilieleza kuwa Kiwanga amepumzishwa kwa saa sita na hivyo Mahakama iliahirisha
kesi hiyo hadi Mei 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment