Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA) Mhe,
Freeman Mbowe amefunguka na kutoa neno kuhusu madiwani 46 ambao
wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
kusema kuwa jambo hilo linafanywa na CCM kwa lengo la kuwakatisha tamaa
wana CHADEMA.
Mbowe amesema kuwa wapo watu wanadhani kitendo cha baadhi ya madiwani
kuhama CHADEMA na kwenda CCM ni kukiuwa chama hicho na kusema suala hilo
haliwezi kutokea kwani madiwani wa CHADEMA nchi nzima wapo zaidi ya
1130 huku madiwani 46 ndiyo waliohama na kwenda CCM na kusema kitendo
hicho kinawapa funzo katika maandalizi ya kutafuta viongozi ambao kweli
wanaweza kukisimamia chama na si wale wanaotafuta fursa za kutoka
kupitia uongozi.
"Kazi kubwa inayofanywa na CCM ni kuwakatisha tamaa na jambo ambalo
limefanyika karibuni ambalo linaonekana wana CHADEMA wengi wamerudishwa
nyuma basi ni suala la madiwani, madiwani wamenunuliwa jamanii wanaunga
mkono juhudi, kuna watu wengine ni mizigo lakini sasa tunafanyaje lakini
watu wa CHADEMA wanakata tamaa eti madiwani wanaisha chama kinakufa,
hiki chama hakifi mzee CHADEMA nchi nzima ina madiwani 1184 madiwani
mpaka dakika hii wameondoka ni madiwani 46 kwa hiyo tuna madiwani zaidi
ya 1130 wamebaki CHADEMA halafu mtu anasema CHADEMA inakufa una akili
wewe?
Aidha Mbowe amesema kuwa hao viongozi ambao wanahama kutoka CHADEMA na
kwenda CCM kwao ni kama funzo kwamba wapo viongozi na watu mbalimbali
ambao wapo ndani ya CHADEMA kwa lengo la kutafuta fursa tu na
wanapoikosa hiyo fursa na ulaji wanaamua kuondoka.
"Kwetu ni funzo tunapojiandaa kwenda kwenye uchaguzi wa Wenyeviti wa
Mtaa, Vijiji, madiwani, wabunge hata nafasi ya Urais tukajiandaa na kina
nani wanaoishi ndoto ya CHADEMA lazima safari hii tujiridhishe mapema
huyu tukimpa nafasi basi historia yake tunaijua vyema" alisema Mbowe
No comments:
Post a Comment