Serikali kupitia Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony
Mavunde,imesema kwamba haijaweka zuio kwa vyama vya siasa kufanya siasa,
bali kuna sheria ambazo zinapelekea kutokea kwa hali hiyo.
Akijibu swali Bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Kazi,
Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, amesema seikali haijuzia vyama vya
siasa kufanya siasa, kwani imevipa uhuru vyama hivyo kufanya shughuli
zake za kisiasa, isipokuwa kuna sheria za jeshi la polisi ndizo zinatoa
muongozo juu ya ufanyikaji wa mikutano ya siasa na maandamano.
“"Si kweli kwamba serikali inazuia harakati za kisiasa, sheria imetoa
uhuru kwa vyama kutafuta wanachama na kufanya mikutano lakini iko
subject na sheria nyinginezo, ikiwemo sheria ya Police force na
auxiliary service act ambayo pia imeweka masharti katika section namba
44 na 45 ya namna vyama vya siasa vinaweza vikafanya kazi zao hasa
katika mikutano na maandamano mbali mbali”, amesema Anthony Mavunde.
Swali lililojibiwa lililoulizwa na Mbunge wa Rombo Joseph Selasini
ambalo lilitaka serikali kusimamia sheria ikiwemo inayowaruhusu
wanasiasa kufanya siasa.
No comments:
Post a Comment