HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 22 December 2017

VPL TANZANIA BARA..SINGIDA YAIMARISHA KIKOSI CHAKE KWA KUSAJILI BEKI KUTOKA GHANA.


TIMU ya Singida imeimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki wa Mghana, Malik Antri ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya wachezaji wa nyumbani kwa ajili ya michuano ya CHAN.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo imesema kwamba Antri amekwishawasili nchini tayari kuitumikia Singida United ambayo inapambana kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika msimu wa kwanza tangu wapande.

Amesema kwamba Antri anachukua nafasi ya Elisha Muroiwa aliyerejea kwao Zimbabwe kufuatia matatizo ya kifamilia yanayomsumbua.

Antri anakuwa mchezaji wa nane kusajiliwa dirisha dogo Singida United, baada ya washambuliaji Daniel Lyanga kutoka Fanja ya Oman, Kambale Salita 'Papy Kambale' kutoka Etincelles ya Rwanda na Lubinda Mundia kwa mkopo kutoka Res Arrows ya Zambia.

Wengine ni chipukizi Issa Makamba, Assad Juma, Ally Ng’azi na Mohamed Abdallah waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za U-17 Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.

Singida United inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 11.

Singida inazidiwa pointi tatu na Simba na Azam na mbili na mabingwa watetezi, Yanga.  Na baada ya mapumziko ya wiki tatu kupisha michuano ya CECAFA Challenge Singida itawafuata Njombe Mji FC Desemba 31 Uwanja wa Saba Saba huko Njombe, mchezo utakaoanza Saa 8:00 mchana.

No comments:

Post a Comment