
Mwinyi alionesha uwezo mkubwa kwenye
michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika Kenya wakati akiitumikia timu ya
taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ na kuisaidia kikosi hicho kumaliza nafasi
ya pili baada ya kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Kenya.
“Ni kweli nimeandika barua kuomba kuondoka
Yanga kwa sababu sipati nafasi ya kucheza”
“Mimi ninaamini nina uwezo mkubwa lakini
nashangaa nimeendelea kukaa nje kwa muda mrefu. Kama unakumbuka nimecheza mechi
nyingi msimu uliopita kuanzia VPL, FA, na hata michuano ya CAF iweje leo
kiwango kimeshuka hadi kukosa kabisa nafasi?”
“Namshukuru sana kocha wangu wa timu ya
taifa ya Zanzibar Hemed Morocco kwa kuniamini na kuniita kwenye kikosi chake
kisha kunipa nafasi, hii inaonesha ni namna gani alivyokuwa na imani na uwezo
wangu.
No comments:
Post a Comment