HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 22 December 2017

MISA YA KRISMAS KITAIFA KUFANYIKA ZANZIBAR IKIONGOZWA NA MHASHAMU ASKOFU AUGUSTINO SHAO


Dar es Salaam. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema misa ya Krismasi kitaifa itaadhimishwa katika Jimbo Katoliki Zanzibar katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Minara Miwili.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi Desemba 21,2017 na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Jamii ya baraza hilo, Bernard James imesema misa hiyo itaongozwa na Askofu wa jimbo hilo, Mhashamu Augustino Shao.

Katika sikukuu hiyo inayoadhimishwa Desemba 25 ya kila mwaka, Wakristo duniani huadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Awali, mratibu wa matukio ya kanisa Tumaini Media, John Leveti amesema Kardinali Polycarp Pengo ataongoza misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam.

"Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa yeye siku hiyo ya mkesha, Desemba 24 ataongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph," alisema Leveti.

"Siku ya sikukuu Kardinali Pengo atafanya ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na Nzigilwa atakuwa St Peters," amesema.

No comments:

Post a Comment