Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa
kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ambalo linaweza kufika eneo
lolote la Marekani.
Runinga ya kitaifa nchini humo imesema kuwa Pyongyang
sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.
Kombora hilo kwa jina Hwasong-15 ambalo imesema ndio
kombora lenye uwezo mkubwa lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano.
Lilianguka katika maji ya Japan lakini liliweza kuruka
juu zaidi ya kombora jingine lolote la taifa hilo .
Rais
wa Marekani Donald Trump ameonya vitisho kutoka kwa mataifa Korea kaskazini na
Iran katika hotuba yake katika umoja wa mataifa.
Katika hotuba yake ya kwanza katika mkutano wa umja huo
mjini New York, ameonya kuwa Marekani itaangamiza Korea kaskazini iwapo
italazimika kujitetea ama kuwalinda washirika wake.
Alimkejeli kiongozi wa Korea kaskazinmi Kim Jong un
akisema: Yuko katika harakati za ''kujitoa muhanga''.
Korea kaskazini imefanya makombora yake kinyuklia
majaribio na kukiuka maamuzi ya Umoja wa mataifa.
Iran, bwana Trump alisema ni nchi ya kifisadi na
inayoongozwa kidikteta kwa lengo la kutaka kuyumbisha eneo la mashariki ya
kati.
Jeshi
la Marekani limerusha ndege yake ya kuangusha mabomu aina ya B-1B katika anga
ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua
inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya
Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo
linaloweza kushambulia nchini Marekani.
Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu
kuonyesha ubabe baada ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini au majaribio
ya mabomu ya nyuklia.
Korea Kaskazini yarusha kombora 'lililoruka juu zaidi'

Taifa la Korea Kaskazini limefanyia majaribio kombora
lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kombora hilo tayari limeonekana
kuhatarisha usalama duniani kulingana na waziri wa maswala ya ulinzi nchini
Marekani James Mattis.
Jaribio hilo la kombora mapema siku ya Jumatano lilianguka
katika maji ya Japan.
Liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali
wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini.
Ni jaribio la hivi karibuni ambalo limezua hali ya
wasiwasi.
Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora
lake ni mwezi Septemba.
Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la
nguvu za kinyuklia mwezi huo.
Urusi yadai Marekani inaichokoza Korea Kaskazini

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amedai
Marekani ndiyo imekuwa ikiichokoza Korea Kaskazini na kuichochea kuongeza kasi
mpango wake wa silaha za nyuklia.
Amepuuzilia mbali wito kutoka kwa balozi wa Marekani
katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kuvunja uhusiano na Korea
Kaskazini.
Hii ni baada ya Pyongyang kufanyia majaribio kombora
jingine.
Urusi imekuwa ikisema kwamba vikwazo na hatua nyingine za
kuiadhibu Korea Kaskazini haziwezi kufanikiwa. Badala yake imekuwa ikihimiza
kuwepo mashauriano.
Marekani imetahadharisha kwamba serikali ya Korea
Kaskazini "itaangamizwa kabisa" iwapo vita vitazuka.
Trump: Japan itayatungua makombora ya Korea Kaskazini
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Japan
itatungua makombora ya Korea Kaskazini, kwa kutumia mitambo ya kijeshi
iliyonunuliwa kutoka Marekani.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema
kwamba, taifa lake litatungua makombora hayo kabla ya kutua ardhini,
"ikiwa hilo litahitajika".
Viongozi hao wawili, walisema hayo walipozungumza na
waandishi habari wakati wa kumalizika rasmi kwa ziara ya kwanza ya kitaifa ya
Bwana Trump nchini Japan.
Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imerusha
makombora mawili hatari juu ya mipaka ya Japan.
China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini
Uchina
imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa
ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo
kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa
na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana
raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo
ambao hauna doria ya kutosha.
No comments:
Post a Comment