
Klabu
ya Simba SC, kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili imetangaza kusitisha
mpango wa kuwasajili kiungo Mzambia, Jonas Sakuwaha na mshambuliaji na Antonio
Dayo Domingos kutoka Msumbiji.
Hans Poppe amesema kwamba katika dirisha
hili dogo Simba imeachana na wachezaji hao na kusajili mchezaji mmoja tu wa
kigeni ili kuimarisha kikosi chake.
Poppe amemtaja mchezaji aliyeachwa
kuwa ni beki Mzimbabwe Method Mwanjali na anayesajiliwa ni Mghana, Asante
Kwasi kutoka Lipuli ya Iringa, akasisitiza kuwa Jamal Mnyate amekwenda Lipuli
kwa mkopo.
Kuhusu mchezaji Domingos, Hans Poppe amesema
mipango ya usajili wake haikukamilika.
Taarifa za awali zilidai kwa Simba
ingewaacha wachezaji watatu na kusajili watatu wapya wa kigeni, wachezaji hao
walikuwa ni Mghana Nicholas Gyan, Mrundi Laudit Mavugo na Mwanjali ambaye
aliachwa kabla, ili kuwasajili watatu ambao ni Asante Kwasi, Sakuwaha na
Domingos.
No comments:
Post a Comment