
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais – TAMISEMI Seleman Jafo jana ametangaza ajira mpya kwa walimu ili kuziba nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi na
walimu katika shule za Msingi na Sekondari waliobainika kuwa na vyeti vya
kughushi.
Akiongea na
waandishi wa habari Jafo amesema baada ya uhakiki wa maombi yalitumwa, jumla
3,033 wamechaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi, kati yao walimu 266 ni wa
sekondari na 2,767 ni wa shule zaMsingi.
Walimu watatakiwa kuripoti katika ofisi za
Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa na kisha kwenda kuripoti katika shule
walizopangiwa, walimu wanatakiwa kuripoti December 27, 2017 hadi January 17,
2018 wakiwa na vyeti vyao,” – Jafo
No comments:
Post a Comment