
Kamati
ya utendaji ya Yanga Ijumaa Desemba 22, 2017, imetangaza majina ya wajumbe sita
iliyowateua kusimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.
Kaimu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga
amesema kamati hiyo ambayo tayari imeshaanza mchakato huo, itaongozwa na
Mwenyekiti, Wakili Alex Mgongolwa ambaye pia ni mwanasheria wa klabu hiyo.
Wajumbe wengine watano wa kamati hiyo ni
aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Profesa Mgongo
Fimbo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya katiba na sheria za ardhi na George
Fumbuka , mtaalamu wa masuala ya uwekezaji.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Felix
Mrema ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya fedha na uchumi sambama na
Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango wa Yanga, Mohammed Nyengi "Sisi
kama uongozi tuna imani kamati hii itafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kwa
sababu inaundwa na wajumbe wenye utaalamu wa hali ya juu ya masuala ya uwekezaji
na pia wana mapenzi na klabu yetu," alisema Sanga.
Miaka 10 iliyopita Yanga ilianza mchakato wa
uuzwajiwa wa hisa zake kwa muhtasari huu unaainisha ufafanuzi wa kazi na
mapendekezo ya kamati maalumu iliyopitia rasmu ya uuzaji wa hisa kwa kampuni ya
Advertisement (Public Company) kulingana na muafaka uliofikiwa na wanayanga
mnamo 22/6/2006.
Katika muafaka huu wana –yanga walikubaliana
kuwa kitu kimoja na kwamba kuwepo Kwa klabu na Kampuni ya umma (Public Company)
ambayo wanachama watakuwa na Hisa na sauti, tofauti na muundo wa kampuni ya
hapo awali ambayo ilikuwa ya binafsi (Private Company).
Katika kufanikisha masuala ya uanzishwaji wa
kampuni ya umma (Public Company) na masuala yote ya hisa watu watatu kutoka
kila kundi (miongoni mwa makundi matatu yaliyokuwepo kabla ya kufikia muafaka
ambayo ni yanga kampuni , yanga asili na yanga academia) waliteuliwa kama
wawakilishi wa makundi wa makundi yao.
Kazi ya kamati hii maalumu ya watu watatu
zilikuwa mbili, kwanza kuandaa rasimu ya kampuni ya umma na pili kuandaa
mchanganuo mzima wa utekelezaji wa muafaka kwa vitendo ambayo itawasilishwa kwa
wanachama na yalihitaji muda wa kutosha kuyapitia.
Kifungu kwa kifungu ili kuhakikisha kwamba
inakidhi matakwa ya kampuni ya umma (Public Company) kama unavyoagiza muafaka
na kukidhi matakwa ya kisheria.
Hata hivyo; mpango huo ulishindikana hadi
mwaka huu ambako umeanza tena na sasa imeundwa kamati nyingine ya watu saba.
No comments:
Post a Comment