HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 24 May 2017

TATHMINI YA MADHARA YA MVUA TANGA YAONESHA WATU 10 WAMEPOTEZA MAISHA MPAKA SASA.

Tathmini ya madhara yaliyotokana na na mvua zilizonyesha kwa siku sita mfululizo wiki iliyopita mkoani hapa zimeonyesha kuwa hadi sasa watu 10 wamekufa huku  nyumba 44 zikibomoka na nyingine 218 zikizingirwa na maji.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ametoa  taarifa ya tahmini hiyo, Jumanne wiki hii wakati akizumgumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Wakulyamba amesema katika yaliyotokena na mvua hizo, watu 10 walimepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, kuangukiwa nyumba na kutumbukia kwenye mashimo  ambapo  saba kati yao  walikuwa wakazi wa Wilaya ya Korogwe, wawili Muheza na mwingine ni mkazi wa Jiji la Tanga huku 20  wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, nyumba 44  ziliezuliwa paa, 218 zilizingirwa na maji, 12 zikisombwa na mafuriko.

Amesema wilaya zilizoathirika zaidi ni Korogwe,Tanga na Lushoto huku Pangani,Mkinga na Handeni zikipata athari  ndogo.

Kamanda huyo alisema katika mafuriko hayo,barabara zilizopo katika za Wilaya mbalimbali mkoani Tanga,zimeathirika kwa kubomoka,kuvunjika makaravati pamaoja na madaraja.

"Kama mnavyoona mvua bado zinaendelea, nawatahadharisha wanaokaa kwenye nyumba zilizopo mabondeni wasisubiri maji yaingie ili waokolewe, kuna wakati mwingine uokoaji unaweza kutofanikiwa na kujikuta mnaangamia,"amesema Wakulyamba.



No comments:

Post a Comment