JESHI la Polisi Mkoani Tanga limedai kukamata
sila tano ikiwemo gobore moja wakati wa Operesheni maalumu ya kuwasaka wahalifu
katika Wilaya ya Kilindi na Handeni.
Akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake, Kamanda Wa Polisi Mkoani Tanga Benedict Wakulyamba (Pichani Juu) amesema kuwa masako huo ulifanywa
kwa siku sita kwa ushirikiano na wananchi.
Amesema wakati wa
operesheni hiyo inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza silaha za
kienyeji pamoja na mitambo ya utengenezaji wa pombe haramu ya Gongo.
Kamanda Wakulyamba
amewataka wananchi kutoa taarifa za kihalifu katika maeneo yao ikiwa na pamoja
na kuwafichua watengenezaji wa Gongo.
No comments:
Post a Comment