
Chama cha Mawakala na
Makarani wa Usafiri wa Abiria jijini Dar es Salaam umesema hautambui mgomo wa
wamiliki wa vyombo vya usafiri uliotangazwa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi
nchini TABOA uliopangwa kufanyika keshokutwa Jumanne.
Chama
hicho kimepinga mgomo huo kwa maelezo kuwa mgomo huo haukufuata misingi ya
uendeshaji wa huduma za usafiri.
Akizungumza
katika mahojiano na KURASA ya EATV katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo hii
leo; Mwenyekiti wa Mawakala na Makarani hao Bw. Khamisi Juma Iddi amesema
kinachofanywa na wamiliki wa mabasi ni sawa na kuanzisha utawala ndani ya
utawala pasipo kujali wadau wengine muhimu katika sekta ya usafirishaji.
Bw.
Juma Iddi amesema wao kama mawakala na makarani wataendeleo kutoa huduma kama
kawaida huku akiisihi serikali kuwa makini na wamiliki wa vyombo vya
usafirishaji abiria kutokana na kile alichodai kuwa ni mwenendo wao unaotia
mashaka.
No comments:
Post a Comment