Chama cha Mapinduzi
CCM kimekemea taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa
wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zenye lengo la kukejeli,
kudhihaki, kukatisha tama, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na chama
hicho na Serikali zake katika kuleta maendeleo kwa watanzania.
Taarifa
ya Chama hicho iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari na Mjumbe wa kamati kuu (NEC)
na msemaji wa chama hicho Christopher Ole Sendeka inasema yapo magazeti mawili
ya nje ya nchi ambayo hutoa makala kila baada ya miezi miwili zinazopotosha na
kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania.
Amesema
mbali na magazenti ya nje pia yapo mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa
makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kuichafua nchi na Rais wake Dkt John
Pombe Magufuli.
Ole
Sendeka amesema chama hicho kinatoa wito kwa vyama vingine vya siasa nchini
kutochukulia kwa wepesi maswala ya Demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo
za kuburudisha au kutoa matumaini hewa kwa wanachama na wananchi.

No comments:
Post a Comment