| Promota Jay Msangi (wa tatu kutoka kushoto waliokaa) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapambano hayo. |
| Mabondia Dullah Mbabe na Cheng Bo Zheng wakizungumza na waandishi wa Habari kuelekea mpambano wao. |
| Mabondia Cosmas Cheka na Jason Bedmen wakizungumza na waandishi wa habari. |
| Afisa Maudhui wa Star Times akuzungumzia udhamini wao kwenye mapambano hayo. |
Macho na masikio ya
Mashabiki na wadau wa mchezo wa masumbwi Afrika Mashariki na kati Okt 27 mwaka
hu yataelekezwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar Es Salaam pale
Bondia mtanzania anayekuja kwa kasi nchini Dulla Mbabe anatapo mkabili Bondia
kutoka nchini China Cheng Bo Zheng, kwenye pambano la kimataifa la raundi 12.
Akizungumza
na Mtandao huu Mkurugenzi wa mpuni ya Hall of Fame Boxing
Promotion Company, Jay Msangi amesema siku hiyo pia wadau na mashabiki wa
masumbwi watashuhudia mpambano mwingine wa kihistoria kati ya Bondia machachari
wa Tanzania Cosmas Cheka, mdogo wake na bondia maarufu nchini Francis Ceka
ambaye atapanda ulingoni kumkabili bondia kutoa Afrika ya Kusini Jason Bedmen
mpambano wa raundi 10.
Bondia
Cosmas Cheka alizingumza na mtandao huu juu ya maandalizi yake kuelekea
mpambano huo huku swali la msingi likiwa ni… Pambano limekuja kwake ghafla Je
amejiaanda vya kutosha na nini anawaahidi watanzania..???
“Mimi
ni askari muda wote niko tayari, nafanya mazoezi kila siku, najua mabondia
wengi wa tanzania ni waoga lakini mimi ngumi ni kazi yangu inayonilisha kwahiyo
muda wote niko tayari, nitampiga tu, hii ni rangi tu, leo ni mweupe lakini
kesho huyu atakuwa mwekundu, sisi wamakonde tuna msemo usemao madengo ntiima
yaani kazi ni moyo” alisema Cosmas Cheka.
Naye
Bondia Dulla Mbabe alizungumzia maandalizi yake kuelekea mpambao huo pambeni
yake akiwemo bondia kutoka china Cheng Bo Zheng.
“wengi
mnafahamu uwezo wangu, na mnakumbuka nilichomfanya Mada Maugo, huyu
ameyakanyaga, mwenzie nilimfuata hukohuko nadhani huyu aliona na sasa
ameyakanyaga mpira unadunda lakini sio kwenye matope”
Mabondia
wote watakao panda ulingoni hapo Okt 28 tayari wamepima uzito na majibu kuwekwa
hadharani,
Jason Bedmen kg 64.6 vs
Cosmas Cheka kg 64.5
Cheng Bo Zheng kg 78.7 vs
Dulla Mbabe kg 77.5
Mapambano
ya utangulizi
Said Mbelwa vs Thomas
Mashali
Shabani Kao vs Paul Kamata
Kurwa Bushiri vs Adamu
Ngange
Mapambano hayo yataoneshwa Live na King'amuzi cha Star Times kupitia chaneli ya SIBUKA MAISHA na kurudiwa na TBC2.
Mapambano hayo yataoneshwa Live na King'amuzi cha Star Times kupitia chaneli ya SIBUKA MAISHA na kurudiwa na TBC2.
No comments:
Post a Comment