HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 13 September 2016

WAZIRI MBARAWA AMWAGIZA MKUU WA MKOA WA TANGA KUSIMAMIA ULIPAJI FIDIA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Maritini Shegella kusimamia ulipaji we fidia kwa watakaopisha Mradi wa bomba la Mafuta litakalo jengwa kutoka Mkoani Tanga kwenda nchini Uganda.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo  wakati akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na maofisa wa Bandari ya Tanga wakati wa ziara yake mwishoni wa wiki mkoani hapa na kupewa taarifa juu ya Mradi wa bomba la Mafuta kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Maritini Shegella.

Amesema mradi huo ni Wawatanzania wote na sio watu wachache ambao watataka kuuhujumu na kujinufaisha wenyewe.

Aidha Mkuu wa Mkoa Maritini Shegella amemuomba Waziri kuwasaidia upatikanaji wa vifaa  katika Bandari ya Tanga kwani inachangamoto ya Wateja huchukuwa muda mrefu hivyo kuchelewesha maendeleo.

No comments:

Post a Comment