HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 14 September 2016

SUNGURA CEMENT WALIA UHABA WA NISHATI TANGA





Licha ya Serikali kuonyesha nia ya kufufua viwanda katika mkoa wa
Tanga bado wawekezaji wengi wa viwanda hivyo wanalalamikia changamoto
za uhaba wa nishati ya umeme pamoja na miundombinu ya reli.

Malalamiko hayo yametolewa na Mkurungenzi Mtendaji  wa kiwanda cha
kuzalisha Saruji cha Sungura,Fauzi Tamimu Wakati akiongea na Mtandao huu
kuhusu changamoto za ukuaji wa sekta hiyo mkoani hapa.

Alisema kuwa iwapo huduma ya umeme itaweza kuimarishwa na kuwa ya
uhakikia wawekezaji wengi wataweza kuja kuwekeza katika mkoa huo kwani
unamalighafi nyingi kwa ajili yaviwanda mbalimbali.

“Umeme kukati kati pamoja na wakati mwingine kuwa mdogo kabisa ni moja
ya vikwanzo vinavyosababisha kusitisha uzalishaji wakati mwingine kwa
kuhofia kuunga mashine hali inayosababisha hasara kubwa kwa
kiwanda”alisema Tamimu

"Kwa Mkoa wa Tanga waone umuhimu wa kupunguza au kumaliza tatizo la
hitilafu ya umeme ,kwani haitakuwa na maana,Mkoa una viwanda vya
Saruji Vingi halafu bei ni sawasawa na maeneo ambayo hakuna kiwanda,"
alisema Mkurugenzi huyo

Akiongela kuhusu miundombinu ya reli alisema kuwa iwapo itaimarishwa
kote nchini itaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa gharama za
usafirishaji wa bidhaa zao wanazizalisha kwenda kwenye masoko.
"Ili maendeleo katika sekta ya viwanda yawepo ni lazima reli ifanye
Kazi kwani itasaidia kupunguza gharama,kwani kwa sasa gharama kubwa
ipo kwenye usafirishaji wa bidhaa" alisema Tamimu.

Hata hivyo Mkurungenzi huyo aliwashauri wazalishaji wa hapa nchini
kuhakikisha wanakuwa na malengo ya kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo
zitaweza kuuzika kwa irahisi hata nje ya nchi.

Tamimu alisema kuwa ni lazima uzalishaji wetu ulenge kuuza katika
masoko ya kidunia baada ya kutegemea masoko ya ndani kwani hapo ndio
tutaona faida ya sekta hiyo.

"Kama bidhaa kutoka nje zinauzika mpaka huku kwetu kwani ni nasie
tusiwe na malengo ya kushika hayo masoko ya kwao ili nchi yetu iweze
kufaidika na fursa hiyo" alisisitiza Mkurugenzi huyo

No comments:

Post a Comment