| Baadhi ya Wakaazi wa Kijiji cha Kilapura wakiwa kwenye foleni ya kuchota maji kwenye bomba moja linalohudumia wakaazi wote wa kijiji hicho. |
BAADHI ya
familia kijiji cha Kirapula kata ya Muungano Wilayani Muheza mkoani hapa wamelazimika
kuyahama makazi yao kufuatia kero ya maji ilichokikumba kijiji chao kwa muda
mrefu.
Pia familia hizo wamesema ndoa zao huingia katika migogoro
kwa kulazimika kuamka saa tisa usiku ili kuwahi foleni ya maji kwenye kisima
kimoja ambacho maji yake hayana uhakika .
“Kero yetu hapa ni ya muda mrefu na viongozi wetu wanajua na
tumekuwa tukipewa ahadi kila siku, kwa sasa subira imezidi na ni bora
kujisalimisha kuepuka magonjwa” alisema Sofia Hassan na kuongeza
“Watoto wetu wamekuwa wakienda shule bila kuoga na nguo
chafu jambo ambalo linawalazimu baada ya kutokuwa na njia mbadala ya kupata
maji na hilo linarudisha nyumba uelewa wa masomo darasani” alisema
Kwa upande wake Diana Hassan, alisema kero hiyo ya maji
imekuwa ikiwaingiza katika migogoro ya ndoa na waume zao baada ya kulazimika
kuamka saa tisa usiku kuwahi foleni katika kisima kimoja kilichopo pekee.
Alisema baadhi ya siku husindikizwa na waume zao na siku
nyengine waume hugoma kuamka jambo ambalo hupelekea kutoka peke yao hivyo
unapochelewa kurejea hupatwa na maswali.
“Kero ya maji inatuingiza katika mizozo na waume zetu kwani
unapochelewa unapatwa na maswali mengi huku ikieleweka wazi kuwa hukumbana na foleni hata uamke saa
nane usiku” a;lisema Diana
Alisema hupata nafuu vipindi vya mvua kwa kuhifadhi katika
mapipa na ndoo na kuepukana na adha ya utafutaji maji usiku na kusema kuwa
endapo ukichelewa unaweza kukosa maji ya kutumia mchana mzima.
Alisema ili kuweza kuzinusuru afya na wakazi wa Kilapula na
kubaki katika makazi yao Serikali kuweza kuwawekea kisima cha maji safi ambacho
watakuwa na uhakika wa upataikanaji na kuepukana na adha ya kuamka usiku wa
manane.
No comments:
Post a Comment