Mkuu wa wilaya ya
Handeni, Mkoani Tanga Mh. Godwin Gondwe ametembelea kambi tiba ya GSM
Foundation yenye lingo la kuokoa watoto zaidi ya 3500 wanaodaiwa kupoteza
maisha kila mwaka kutokana na kuzaliwa na tatizo la vichwa vikubwa na mgongo
wazi.
Inasemekana
zaidi ya Watoto 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka
nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa
asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao
wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa Tiba.
Akizungumza
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga "Bombo" wakati wa zoezi la
Upasuaji wa watoto hao lilipokuwa likiendeshwa na madaktari Bingwa, Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya (MOI)iliyopo Hospitali ya Rufaa
ya Muhimbili, Dkt Othman Kiloloma alisema ongezeko la watoto hao linatokana na
ukosefu wa lishe yenye virutubisho vijulikanavyo kwa jina la “Folic Acid”
Alisema
kukosekana kwa lishe hiyo kumesababisha tatizo hilo kwa watoto ambalo
lisipopatiwa ufumbuzi wa kina linaweza kupelekea athari kubwa kwao ikiwemo vifo
hali inayoweza kupunguza jamii ambayo ingeweza kuchangia ukuaji wa uchumi
katika shughuli za uzalishaji.
“Ukiangalia
kwa hivi sasa zaidi ya watoto wapato 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua
ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo
huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa hivyo jamii inapaswa
inapaswa kuwapeleka katika Hospitali ili kuweza kuchangia ukuaji wao na
maendeleo “Alisema
Akizungumzia
kuhusu changamoto zinazosababisha watoto hao kukosa huduma za upasuaji, Afisa
Habari wa Taasisi ya Afya inayojihusisha na Upasuaji wa watoto hao, Khalfani
Kiwamba alisema kuwa upungufu wa madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa
waathirika hao ni mkubwa kwa sababu nchini wapo saba ambapo sita wapo Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili na mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza
Bugando.
Awali
akizungumza katika zoezi hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Godwin Gondwe
aliipongeza taasisi inayojihusisha kusaidia sekta ya Afya na Elimu hapa nchini
(GSM) kwa kutoa matibabu ya upasuaji huo kwa watoto hali ambayo itawasaidia
kuweza kurejea kwenye hali zao za kawaida.
Alisema
katika suala kama hilo jamii haina budi kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo
hayo badala yake waona namna ya kuwasiliana na viongozi wao ngazi za chini
kuwaepusha na vifo ambavyo vinaweza kuwakumba kutokana na hali walizonazo.
“Lakini
pia lazima jamii ibadilike kuona umuhimu wa kuacha kuwaficha watoto wenye
matatizo hayo badala yake wawapeleke kwenye hospitali zilizopo karibu nao kwa
ajili ya kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kupona “Alisema.
IMETOEWA:SADICK HAMIDU TV via Facebook.
IMETOEWA:SADICK HAMIDU TV via Facebook.

No comments:
Post a Comment