HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
Pages
Thursday, 18 August 2016
MKUU WA WILAYA YA KOROGWE KUWAKAMATA WATENDAJI WA VIJIJI WASIOTOA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI KWA WANANCHI.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Robert Gabriel (pichani) amehaidi kuwachukulia hatua Watendaji wa vijiji ambao hawatasoma taarifa ya mapato na matuminzi kwa Wananchi kuazia hivi sasa jambo ambalo linachangia kuleta migogoro .
Aliyasema hayo Jana wilayani humo alipokuwa akizungumza na wanakijiji wa Mnyuzi amesema tangu kufika hapa ni siku 42 amekuwa akipata malalamiko kutoka kwa Wanachi ikiwemo la kutopatiwa taarifa za mapato na matumizi kwa muda ameongeza kusema nimekuja kuondoa kero za wananchi kwa kushirikiana na watendaji waliopo kwenye ngazi mbalimbali ambapo kwa nafasi yangu ya utendaji mkuu wa watumishi sitokuwa radhi kuona wananchi wakikosa kutendewa haki kwa uzembe wa watu wachache.
DC Gabriel amesema katika mikakati yake ni kuhakikisha wilaya ya Korogwe inakuwa na ongezeko la sekondari za elimu ya juu,amesema wananchi washiriki baadhi ya kazi katika kujenga shule ya sekondari Mnyuzi nasio kutegemea fedha ambazo zimetolewa katika kutekeleza mradi mbalimbali ya huduma za jamii kwa kushirikiana na nguvu za wananchi ambapo miongoni mwa miradi iliyofanyika ni ujenzi wa vyumba vya madarasa,Zahanati kijiji cha Mwenga na Magila Gereza na tenki la maji Old Korogwe.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo George Nyaronga amewataka wananchi kufichua watendaji wazembe ili aweze kuwashughulikia kwa mujibu wa kanuni na sheria amesema kazi hiyo iko kwenye himaya yake na serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Magufuri haitoweza kuwavumilia viongozi wazembe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment