Na Said Killeo TANGA.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi wa migodi,nishati (TAMICO) wametakiwa kuchagua viongozi waliokuwa tayari kuwatumikia wafanyakazi.
Rai hiyo imetolewa jana na mwenyekiti mstaafu wa Tamico taifa Patric Nkwabi wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Tamico uliofanyika jijini hapo amesema viongozi wapya hawana budi kupokea jukumu hilo na kuepuka vitendo vya rushwa ili kuleta maendeleo ya haraka.
Pia Mwenyekiti Nkwabi amesema kuwa hapo nyuma kulijengeka dhana kwamba vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikizusha migogoro kati ya waajili na wafanyakazi kama kuna migogoro ni vema ikatatuliwa kwa kufuata taratibu za sheria.
Nae Katibu Chadau Mkoa wa Tanga Frola Ngeni amesisitiza upatikanaji wa viongozi bora ili kuepuka kutokujuta katika kipindi cha miaka mitano ya kushika madaraka ambapo alihimiza uwapo viongozi wanaojituma kuimarisha chama.
No comments:
Post a Comment