Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (kushoto) akisalimiana na wananchi wa Handeni walio kwenye harakati za kutafuta maji. |
Na.Mwandishi wetu Saidi Killeo kutoka Handeni anaripoti...
Wadaiwa sugu waliolimbikiza madeni ya bili za maji wilayani Handeni wametakiwa kulipa haraka ili kuweza kufanikisha kupatikana kwa huduma ya maji.
Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakati akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Maji safi wilayani humo kwenye ziara yake ya kushitukiza kwenye ofisi za idara hiyo na baadae kutembelea vyanzo vya maji.
Pia DC huyo amesema Idara ya maji inakabiliwa na uhaba wa fedha ila ni kutokana na kuwepo watumiaji wa maji ambao hawalipi hali ambayo imesababisha mamlaka hiyo kudaiwa na Tanesco zaidi ya shilingi 7millioni katika vyanzo mbalimbali hivyo kuzitaka taasisi na idara wanaojijua wanadaiwa walipe haraka ili huduma ya maji ipatikane.
Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Handeni Twaha Mgaya amesema kuwa watatoa fedha hizo mapema mwisho wa mwezi huu bila kusubiri fedha za bajeti Kutokana na unyeti wa huduma hiyo kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (kushoto) akinywa maji ya bomba na wananchi wake. |
No comments:
Post a Comment