MBUNGE wa Jimbo la
Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk (Pichani Kushoto) amefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tanga kujibu shitaka la kutoa maneno ya
uchochezi.
Mbunge
huyo alifikishwa mahakamani hapo saa 8.30 alasiri jana akiambatana na jopo la mawakili
wake wakiongozwa na Warehema Kibaha.
Mbele
ya Kaimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Hilda Lyatuu Wakili
wa Serikali, Saraji Iboru alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 13,
mwaka huu.Iboru
alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kutoa maneno ya uchochezi wakati
akiwa katika mtaa wa Madina jijini Tanga majira ya saa 10 jioni alipokuwa
akihutubia mkutano wa hadhara.
Wakili
Siraji akiwa na mwanasheria mwenzake wa Serikali, Shose Naiman aliendelea kudai
mahakamani hapo kuwa katika mkutano huo, Mbunge huyo alisema Mapango ya Amboni
yanatumika kwenda kuwaua vijana.
Mshitakiwa
huyo alikana shitaka hilo na mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi leo ili kutoa
nafasi kwa upande wa mashtaka na mshitakiwa kukamilisha taratibu za kupata watu
watakaokidhi masharti ya dhamana ambayo yamewekwa na mahakama.
Hata
hivyo, Mbunge Mbarouk pamoja na mambo mengine leo atatakiwa kuripoti mahakamani
hapo akiwa ameambatana na watu wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao ndio
watakuwa na sifa ya kumdhamini katika shitaka hilo.
CHANZO:GAZETI LAHABARI LEO
No comments:
Post a Comment