Na Said Killeo ..TANGA
Kampuni
ya saruji ya Tanga Cement jana ilizindua kinu cha pili cha kuzalisha bidhaa ya
klinka hatua inayotajwa kuwa itakiwezesha kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa
malighafi hiyo muhimu katika utengenezaji wa saruji kutoka tani laki tano kwa
mwaka mpaka kufikia tani milioni moja na laki mbili na nusu (1.25mil).
Akizungumza
katika katika hafla ya uzinduzi wa kinu hicho, Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni
hiyo, Wakili Lawrence Masha, alisema Mradi huo ulioanza Agosti 13, 2013
unajumuisha mtambo wa kuponda mawe chokaa na udongo, mtambo wa kuchanganyia
mawe chokaa na udongo, mtambo wa kusaga mchanganyiko wa udongo na mawe chokaa,
pamoja na mtambo wa kusaga makaa ya mawe.
Alisema
gharama za ujenzi wa mradi huo mpaka kukamilika ni kiasi cha dola za kimarekani
milioni 152 huku akiongeza kuwa majaribio ya uzalishaji wa klinka ya kwanza
kutoka kinu hicho kipya yalifanyika Disemba 10 mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment