Diwani Omari Masoud (CUF) "wa kwanza kushoto" |
Wananchi Wa Kata ya
Mabanda kijiji cha Misima tarafa ya Sindeni Wilayani Handeni Mkoani Tanga
kwanyakati tofauti wamempongeza Diwani wao kwakutekeleza ahadi ya kuweka umeme
katika Zahanati ya Misima.
Wakizungumza
na kituo hichi Wananchi hao wamesema Wanamshukuru Diwani Omari Masoud
(CUF) kwakuwawekea umeme kwani walikuwa wanapata adha ya kupata Huduma nyakati za
usiku wanaladhimika kutumia vibatali pamoja na simu.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Mabanda Omari Masoud amesema kuwa anawaomba
wananchi Wa Kijiji cha Misima kumuunga Mkono kwa kumpatia ushirikiano katika
kuhakikisha wanaleta maendeleo kwani wananchi akiwa hawapati Huduma nzuri ya
kiafya hatuwezi kuendelea.
Aidha
Diwani Masoud ametoa wito kwa Wananchi kujiunga katika mfuko Wa bima ya
Afya wajamii Wa CHF kwakuwa utakuwa mkombozi kwa kuwapatia matibabu kwakuwa
Huduma hiyo ni yatelekwate kwa mwananchama.
No comments:
Post a Comment