Na. SAID KILEO ..Lushoto.TANGA
Mkuu wa mkoa wa Tanga,Martin Shigella (pichani kushoto)ameuagiza uongozi wa halmashauri
ya Wilaya ya Lushoto kuhakikisha kiasi cha fedha shs. 128 mil zilizowasilishwa
MSD kwa ununuzi wa madawa zinalejeshwa katika mikono salama ili kuweka
utaratibu.
Shigella ametoa agizo hilo juzi kwenye kikao cha
baraza la madiwani kilicholenga kuwasilishwa hoja za mdhibiti na mkaguzi wa
hesabu za serikali kilichofanyika wilayani Lushoto.
Agizo hilo la mkuu wa mkoa limekuja baada ya hoja
za madiwani walioshauri fedha ambazo ziliwasilishwa MSD ili kupata dawa ambazo
mpaka sasa hazijapatikana kuielekeza bohari ya madawa kupata huduma eneo
jingine.
Katika kikao hicho, Diwani wa Kwemshasha,Anuary
Abdassi amesema ni vyema fedha zilizopelekwa MSD ambazo mpaka sasa hazijapata
mrejesho wa kuletwa kwa dawa na hazijapatikana ni vyema wahusika wakafanya
mpango kupata dawa sehemu nyingine ili wananchi wasiweze kuathirika.
No comments:
Post a Comment