Kwa mujibu wa
Wikipedia, Robert Pershing Wadlow, ambaye ameishi kati ya February 22, 1918 na
July 15, 1940, ambaye pia alijulikana kama Jitu la Alton na jitu kubwa la Illinois, alikuwa ndiye mtu mrefu aliyewahi
kuwekwa katika kumbukumbu za Kitabu cha kumbukumbu za Guiness.
Urefu
wa Wadlow ulifika futi 8 na inchi 11.1 au sentimita 2.72 na alikuwa
na uzito wa pauni 439 au kilo199 wakati wa kifo chake akiwa naumri wa
miaka 22.
Kisayansi
umbile lake kubwa kuendelea kukua kwake wakati wa utu uzima umetokana kuwepo
kwaukuajiusio wa kawaida unaotokana na kuongezeka kwa seli katika kiungo
kiitwacho pituitary gland,kitu
ambacho kinasabaisha kuwepo kwa kiasi kikubwa cha homoni za ukuaji. Hakuonesha
kuacha kukua hata wakati a kifo chake
Mtu
huyo alikuwa na urefu wa futi tatu alipokuwa mtoto anliweza kumbeba baba yake
alipokuwa na umri wa miaka tisa. Mikono ya Wadlow iliweza kufikia futi tisa na
inchi tano ikipanuliwa na viganja vyake violikuwa na ukubwa wa futi moja.
Wadlow's
alipofariki jeneza lake likuwa na uzito wa pauni 1,000 na lilihitaji wabebaji
18 ambao walilibeba kulifikisha mahali pake pa mapumziko ya mwisho Alton,
Illinois. Familia ya Wadlow iliamua kuharibu vitu vyake kwa hofu kuwa vinaweza
kukusanywa na kuenyesha katika maionyesha kana vitu vya ajabu vya kumbukumbu
Hata
hivyo, utafiti wa miaka 16 uliofanyika huko Handeni unaonyesha kuwa Tanzania
inaweza kuwa na historia ya mtu mrefu zaidi duniani.
Katika
hali ya kawaid si rahisi kuamini kuwa kuna mtu mwenye urefu wa futi 35, lakini
utafiti wa hivi karibuni umegundua kitu ambacho kimeelezwa kuwa ni ajabu sana
juu ya maajabu hayo
Huko katika cha Ngwujini, wilayani Handeni
mtafiti mmoja wa mambo ya kale na ya asili, Ramadhani Ayubu amegundua kitu cha
ajabu. Mtafiti huyo ambaye amefanya kazi yake hiyo kwa miaka 16 amgundua kaburi
lamtu mmoja wa ajabu ajulikanaye kwa jina la Mbulushi Malilo.
Mtu huyo ambaye kaburi lake lilipimwa na
kufikia futi 35 anaelezwa kuwa mtu waajabu sana alieyishi katika karne ya 16
ambaye alikuwa na nguvu za ajabu. Kwa mujibu wa Mtafitia Aybu mtu anasemekana
kuwa aliwahi kuchiimba bwawa ambalo hadi sasa linatumika na alikuwa na sauti
kubwa ambapo hata akiita mtu inasikika kwa kilomita moja.
Kwa mujibu wa Ayubu, ambaye anamiliki kampuni
inayoitwa Regulate Body Temperature Cilini iliyoko Amana, jijini Dar es Salaam
mtu huyo anaidaiwa kuwa alikuwa mtaalamu wa masuala ya kivita na alitumika hata
hata katika vita mabvyo watu mashuhuri kama OleTiptip na Bushiri walipigana na
watawala.
Ayubu, ambaye anadai kuwa alisoma
Ethiopia masomo ya Sayansi na akalazimika kuacha kutokana na mgogoro wa mpaka
kati ya Ethiopia na Eritres alidai kuwa kabla hajafa aliweka wosia kuwa lazima
akifa azikwe Ngugwini.
Akielezea namna alvyofahamu juu ya hadithi za
mtu huyo, mtafiti huyo wa mambo ya mazingira na mambo ya kale, alisema kuwa
alipata kujua habari zamtu mtu kutoka kwa watu wa familia ya Mbulushi ambao
alikutana nao Same, mkoani Kilimanjaro. Alielezwa kuwa katika kaburi lake
alikuwa amezikwa na mkuki wake.
“Ndipo nilipoamua kwenda huko Ngwujini lakini
nilipopata taabu sana kwa sababu wanakijiji walikuwa wanaona ajabu mimi
kufuatilia kaburi ambalo walikuwa wanaliona kama kaburi la kawaida sana,”
alisema Ayubu ambaye alisema kuwa imechukua miaka 16 kwa wanakijiji hao
kukubali kuwa kaburi ni la mtu wa ajabu sana.
Alisema kuwa vijana, wazee na wanawake baada
ya ugunduzi huo walikuwa hawaamini na wanauliza kwa nini kaburi, kama ni la mtu
wa ajabu halijulikani. Wanasema kuwa hawaoni kuwa kuna faida yoyote kwa kuwepo
kwa kaburi hilo.
Eneo hilo lenye kaburi linafanywa na wakazi
wa eneo kamaeneo la mizimu na kuna mti wa aina ya mkuyu ambao watu wanaamini
hata ukikatwa utaendelea kusimama hivyo hivyo. Eneo hilo wanakijiji wameamua
kulihifadhi lakini linakabiliwa na tishio la kukatwa kwa miti.
Kwa mujibu wa amtu mmoja aitwaye Omari
Athumani, almaarufu kwa jina la Mganga ambaye ni wa kizazi cha Mbulushi ambao
wanatunza kaburi hilo, hapo mwanzoni kulikuwa na msitu mkubwa. “Miti
ilikuwa inavuma sana lakini hakuna miti. Msitu umekatwa,” alisema
Aliendelea kusema kuwa historia na utamaduni
sasa hivi vimepotea na kudai kuwa kulikuwa na nyani ambaye akipita tu mvua
inanyesha lakini sasa hivi amepotea kutokana na msitu kukatwa.
Mganga pia alieleza kuwa kwenye bwawa ambalo
anadai limechiimbwa na Mbulushi peke yake kuna mamba ambaye hatoki mpaka aitwe.
Naye Sudi Mohamed Mgweno amefafanua zaid
kuhusu mti ambao wanaamini ukikatwa unaendelea kusimama, alisema kuna mwaka
watu kutoka Kenya walikuja kukata miti kwa ajili ya mbao na walikata mti huo.
Amesema kuwa walikata mti huo kwa sababu ulikuwa unavutia kutokana na ukubwa
wake. “Mti huo ulikatwa na kusimama tena,”alisema.
Nao vijana mmoja Swedi Ramadhani na Juma Said
walisema kuwa wanaamini kuwepo kwa kaburi hilo kunaweza kuleta fursa za
maendeleo ambazo hazikuwepo hapo awali pamoja na kuwepo kwa raslimali hiyo ya
watu wa kale.
IMETOLEWA:Tangakumekuchablog
IMETOLEWA:Tangakumekuchablog
Kwa
maelezo zaidi wasiliana na Mvumbuzi Ramadhan Ayoub simu 0717 720221
No comments:
Post a Comment