SERIKALI imesitisha
ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.Kutokana na
uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na
wakala zake pamoja na utoaji wa vibali wa likizo ya bila malipo.
Katibu
Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, (pichani kushoto) jana alisema kuwa Serikali imesitisha kwa
muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake.Alisema
utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa
vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo
Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za
kiutumishi.
“Ni
kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia
ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki.
“…na
hili litakwenda sambamba na hata kusitishwa malipo ya mishahara yanayotokana na
upandishwaji wa vyeo kwa watumishi. Tukimaliza zoezi hili ndipo tunaweza kuanza
kutoa ajira za Serikali,”alisema Dk. Ndumbaro.
Alisema
muundo mpya wa utumishi wa Serikali unakwenda sambamba na uhakiki wa malipo ya
mishahara, hivyo ni lazima ujue ni nani unayemlipa kuliko ilivyo sasa.Kwa
mujibu wa maelekezo hayo uhamisho na uidhinishaji katika mfumo wa watumishi
ambao wamehamishwa kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwajiri mwingine ambao
atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa pia utaangaliwa kwa lengo la kupata
taarifa sahihi za mtumishi husika.
“Baada
ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki watumishi pamoja na tathmini ya muundo wa
Serikali na taasisi zake, wote wataarifiwa ni lini utekelezaji utaendelea,”
alisema.
Taarifa
kutoka maeneo mbalimbali nchini, zinaarifu kuwa maelekezo hayo yalitolewa Juni
13, mwaka huu na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa makatibu wakuu
wote, makatibu tawala wa mikoa, kwa wakuu wa idara za Serikali zinazojitegemea.Waliotakiwa
kutekeleza maelekeo hayo ya Serikali ni wakurugenzi wote wa majiji, manispaa na
miji, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, watendaji wa taasisi za
umma na watendaji wa wakala za Serikali kwa upande wa Tanzania Bara.
Kamatakamata
Wiki
iliyopita vyombo vya dola vilianza kuwatia mbaroni watumishi hewa kwa kuwafuata
na pingu majumbani.Hatua hiyo imetajwa kuwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, kuanza kupambana na watendaji ambao
wamekuwa wakiisababishia hasara Serikali ya kulipa mamilioni ya shilingi kwa
watumishi hewa.
Kutokana
na uamuzi huo ambapo mtumishi mmoja wa moja za Mkoa wa Kigoma, alifuatwa na
askari wa polisi na kutiwa mbaroni nyumbani kwao Ubungo Kibangu jijini Dar e
Salaam.Tukio hilo la aina yake lilitokea mchana wa juzi na kuibua hisia
miongoni mwa majirani ambao waalisema kuwa, askari hao walifika nyumbani kwao
na mtumishi huyo na kumfunga pingu mikono na miguuni na kuondoka naye.
Kutokana
na hekaheka hiyo ya watumishi hewa, taarifa kutoka wilayani Nyasa mkoani
Ruvuma, zilidai kuwa walimu watano wastaafu nao walikamatwa na polisi kwa madai
ya kupokea mishara hewa.Mbali na walimu hao pia alikuwepo muuguzi mmoja.
Hivi
karibuni akizungumza Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema Serikali
imewaondoa jumla ya watumishi 12,246 kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa
sababu mbalimbali, ikiwemo umri wa kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na
kumalizika kwa mikataba.Waziri Kairuki alisema kuondolewa kwa watumishi hao
kumeokoa Sh bilioni 25 ambazo zingelipwa kwa watumishi hao.
Alisema
kuwa fedha hizo zingepotea endapo watumishi wasingeondolewa kwenye mfumo,
ikilinganishwa na watumishi 10, 295 walioondolewa kwenye mfumo kuanzia Machi 15
hadi Aprili 30 mwaka huu.
Alisema
pia kuwa watumishi hewa 1,951 wameongezeka ikiwa ni pamoja na Sh bilioni 1.8.
Alifafanua
kuwa ofisi hiyo ilitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi za umma
na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwasilisha taarifa ya watumishi hewa ifikapo
Juni 10, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment