Wanachama,Wapenzi
pamoja na Wadau Wa timu ya African Sport Club ya jijini Tanga wametakiwa kuweka
pembeni tofauti na viongozi watimu kwa kuweka mbele masilahi ya timu.Wito huo
umetolewa na Mjumbe Wa Kamati Tendaji Godias Kimati (Pichani Kushoto) katika kikao cha
wanachama na viongozi kilicho fanyika Jana kwenye ofisi ya Club hapa jijini
Tanga.
Mwenyekiti
Wa timu Habibu Ezi amesema kupitia kikao cha leo cha Wanachama kitakuwa
kinajenga umoja pia ameahidi kutumia nafasi yake ataunda kamati ndogo
kwajili ya kusaidiana kwakuiboresha Club.
Katika
kikao hicho kilikuwa na Agenda kuu 3
:Agenda ya kwanza kujadili Wanachama
:Agenda ya pili ni kujadili juu ya uchaguzi Wa Viongozi
:Agenda ya tatu ni kujadili juu ya Usajili
:Agenda ya kwanza kujadili Wanachama
:Agenda ya pili ni kujadili juu ya uchaguzi Wa Viongozi
:Agenda ya tatu ni kujadili juu ya Usajili
Ila
Waswahili wamesema kwenye wengi kunakuwa na mengi ndipo agenda ya kwanza ikawa
na vuta in kuvute juu ya kujadili Wanachama kuomba uongozi kupunguza kiwango
cha fomu kuwa shilingi 1000 na Cardi ya uwanachama shilingi 5000 na Ada ya kila
Mwezi kuwa shilingi 1000 kwa kuwatazama wanachama na wapenzi Wa hali ya chini .
Nae
Mwanacha Kombo Saidi katika viwango hivyo ameona haviwezi kuijengea
timu kuwa na kipato hivyo kwamaoni yake amependekeza Ada pamoja na fomu
kiongezwa
Aidha
Mlezi Wa timu Mzee Kisauji amewataka Wanachama na Wapenzi Wa African Sport
kuacha maneno ambayo yatabomoa timu nakuwataka kuliza kwa viongozi kitu ambacho
huja kifahamu vizuri..
No comments:
Post a Comment