WAKAZI wa
kijiji cha Mwanyumba kata ya Bwiti
Tarafa ya Maramba Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, wameitaka Serikali
kurejesha mfumo wa upatikanaji wa maji safi baada ya miundombinu yake kuchakaa.Wakizungumza
na waandishi wa habari juzi, wakazi hao wamesema hali za afya zao ziko
mashakani baada ya kutumia maji ya mto ambayo pia hutumiwa kwa ajili ya
kunyweshea mifugo.
Walisema mbali ya uchakavu huo unapotokea ujio wa viongozi
wa Serikali maji hutoka katika mabomba na kuwapa mashaka juu ya sababu zinazopelekea
kukosekana kwa maji kwa muda mrefu.
“Ajabu hapa tuko na mwaka bomba halitoi maji lakini ujio wa
viongozi wa Serikali imekuwa neema kwetu, tumekuwa tukitumia maji ya mito
ambayo pia hutumiwa na wanyama” alisema Asha Bakary na kuongeza “Usikiapo ujio
wa viongozi wa kitaifa ujue maji
yatatoka ila tatizo hatuna vifaa vya kuhifadhia , ila leo ni sikukuu ya wa watu
wa Mwanyumba” alisema
Alisema kuna tishio
la kuzuka kwa magonjwa ya tumbo na kichocho baada ya wakazi wote kutumia maji
ya mto kwa matumizi ya kunywa kupikia na kuongea wakiwemo wanyama.Akizungumzia
kero hiyo, Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji kata ya Magati, Kimwaga Shauri,
alisema uhaba huo wa maji kijiji cha
Mwanyumba umetokana na vijiji kuongezeka ambapo awali kijiji hicho kilikuwa
hakimo katika mradi wa maji.
Alisema kuongezaka kwa vijiji imekuwa sababu ya baadhi ya
maeneo kukosa maji kwa baadhi wa wakati na kusema kuwa Serikali inafanya
jitihada za kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na maji safi na salama.
“Mradi wakati ulijengwa ulikuwa wa vijiji vitatu na sasa tuko na vijiji saba jambo ambalo
linatupa wakati mgumu kuyagawa na kuzifkia kaya ikiwemo kijiji cha Mwanyumba
ambacho hakikuwemo katika mradi” alisema Shauri
Alisema jitihada za kuhakikisha maji yanapatikana kijijini
kwa kutumia mfumo wa zamu unafanyika na kuwataka wananchi kulinda vyanzo vya
maji na kuacha kukata miti .
No comments:
Post a Comment