Vijana mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza kwa
wingi katika Kongamano la maadili ya kiroho sambamba na uchangiaji
Wa damu kwakuokoa vifo vya Mama na Mtoto ambalo vinatokana na ukosefu wa damu.
Wito
huo umetolewa na Mratibu Wa Huduma ya Vijana na watoto (CYM) Agnes Sameji (pichani kushoto) Jana
katika kituo cha Vijana Novelty cha jimbo la Tanga mjini amesema
Kongamano hilo limeandaliwa na Vijana Wa Free Pentecostal Church of
Tanzania(FPCT) kwa kushirikiana na Taasisi ya Novelty pia kongamano
hilo litahudhuriwa na wawezeshaji kutoka nje ya nchi ikiwemo Kenya
huku mgeni rasmi no Mkuu Wa Mkoa Wa Tanga.
Akizungumza
na kituo hichi Mratibu Wa kituo cha Vijana Novelty Jusson Eliyakim
ameongeza kusema kwakupitia kongamano hilo Vijana watapata Elimu ya
ujasiliama, Utandawazi na elimu ya Afya hivyo amewataka Vijana kujitokeza
kwajili ya kuwasaidia jamii ambayo inaguswa na tatizo la damu.
Aidha Katibu
Wa Huduma ya Vijana na Watoto jumbo la Tanga Gamma Malack amesema mandalizi
yote yamekamilika kwa Vijana ambao watashiriki kwakuwa Vijana watapatiwa
maradhi ,chakula kwa muda wote ambao watakuwa hapo hivyo watachangia
shilingi 20,000 hivyo amewataka Vijana kujitokeza katika kongamano.
No comments:
Post a Comment