Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa
kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na
gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa mara
tatu kwa siku katika hospitali hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha alisema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa.
Kwanini Hospitali imechukua hatua hii
Bw. Aligaesha alisema Hospitali inataka kujikita katika
majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.
“Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha
ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa
kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa
ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku,
kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha
mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu.
"Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku
tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye
usafiri” alisema Bw. Aligaesha
Aliongeza kuwa adha ya pili wanayopata ndugu ni usumbufu
ambapo inabidi kuacha shughuli nyingine za uzalishaji ili kuja kuleta chakula
mara tatu kwa siku, hivyo kuingiliana na shughuli zao za kiuchumi na kimandeleo
na kushindwa kuzalisha. Hivyo jukumu hili linachukuliwa na Hospitali
kuwaondolea adha hii.
“Pia kuna baadhi ya ndugu wamekuwa wakishindwa
kuwaletea chakula wagonjwa wao hivyo hospitali ililazimika kuwapatia chakula
ambacho kilikuwa kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka mikoani wasio na ndugu hapa
Dar Es Salaam” alisisitiza Bw. Aligaesha.
Alisema kumekuwepo na ongezeko la msongamano wa watu ndani
ya Hospitali toka asubuhi saa 12 mpaka saa 12 jioni, suala linaloingiliana na
utoaji huduma hasa saa za mchana kwani muda wa saa 6.00 hadi saa 8.00 mchana
ulikuwa unaingiliana na majukumu ya kiutendaji ambapo majopo mbalimbali ya watalaamu
yamekuwa yakiendelea na raundi za wagonjwa waliolazwa. Hii wakati mwingine
imesababisha mgonjwa kutokupata huduma stahiki kutokana na muingiliano huu.
·
“Vile vile msongamano huu ni changamoto kwa
ajili ya masuala ya kiusalama ambapo kati ya watu wanaoingia Hospitali kwa
kigezo cha kuja kuona wagonjwa kuna wanaoingia kwa lengo la kufanya uhalifu
ikiwemo wizi wa mali za Hospitali, magari pamoja na vifaa vya magari” alisisitiza.
Alisema kwa kufanya hivyo, Hospitali itapunguza baadhi ya
gharama za uagizaji wa vyakula kwa wazabuni, kulinda upotevu na baadhi ya
vyakula kuharibika wakati mwingine kwani utunzaji wa vyakula una mahitaji
makubwa.
Bw. Aligaesha alisema Hospitali inakusudia kutoa chakula
chenye ubora na viwango vinavyotakiwa kwa wagonjwa ikiwemo kutoa chakula
maalumu (special diet) kwa wagonjwa wenye uhitaji huo.
Utaratibu wa chakula cha mzabuni kwa wagonjwa
Kuhusu utaratibu huo Bw. Aligaesha alisema Mzabuni ndiye
atakayepika chakula kwa wagonjwa wote waliolazwa na atatayarisha, atakipeleka
na kukikabidhi katika wodi husika ambapo jukumu la kumpa mgonjwa kifungua
kinywa, chakula cha mchana na jioni linabaki wa Hospitali.
Alisema wagonjwa watapatiwa milo mitatu kwa siku yaani
asubuhi, mchana na jioni kazi itakayofanywa na muuguzi wa zamu ambaye
atahakikisha wagonjwa wote wamepata chakula kufuatana na mahitaji (diet list)
iliyowasilishwa jikoni kutokana na mahitaji yao ya kiafya.
Muda wa kuona wagonjwa
Kutokana na uamuzi huu, utaratibu wa ndugu kuleta chakula
kwa wagonjwa waliolazwa wakati wa mchana umefutwa na hivyo mchana hatutakuwa na
nafasi ya ndugu kuja kutembelea wagonjwa. M
uda wa kutembelea wagonjwa utakuwa asubuhi saa 12 hadi saa moja kamili na saa 10:00 jioni hadi saa 12:00jioni ndipo ndugu wataruhusiwa kuingia ndani kuwaona ndugu zao waliolazwa. Katika muda huo ndugu ataruhusiwa kuja na chakula chochote anachofikiri atamuongezea mgonjwa wake kama matunda n.k
uda wa kutembelea wagonjwa utakuwa asubuhi saa 12 hadi saa moja kamili na saa 10:00 jioni hadi saa 12:00jioni ndipo ndugu wataruhusiwa kuingia ndani kuwaona ndugu zao waliolazwa. Katika muda huo ndugu ataruhusiwa kuja na chakula chochote anachofikiri atamuongezea mgonjwa wake kama matunda n.k
Uchangiaji huduma ya chakula
Bw. Aligaesha alisema mgonjwa aliyelazwa atachangia kiasi
cha shilingi 50,000 atakapolazwa ambapo kati ya hizo, shilingi elfu 10,000
itakuwa ni gharama ya kumuona daktari (Consultation), shilingi elfu 10,000
ikiwa ni gharama ya kulazwa na bei ya chakula itakuwa shilingi elfu 30,000 sawa
na shilingi elfu 6,000 kwa siku. Wastani wa mgonjwa kukaa wodini ni siku tano.
Gharama hizo zinahusika kwa muda wote atakaokuwa amelazwa.
Kwa sasa Hospitali inatoa chakula kwa wagonjwa 650 ambao
wamepata rufaa kutoka hospitali za nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama
wastani wa shilingi 1.8 bilioni kwa mwaka, sawa na shilingi 150 milioni kwa
mwezi kwa vyakula pamoja na gharama nyingine kama vile za nishati.
Takribani wagonjwa kati ya 600 na 700 ambao rufaa zao ni kutoka Hospitali za Dar es Salaam walikuwa hawapati chakula kutoka Hospitalini, na ilibidi ndugu zao wawaletee chakula. Hata hivyo, Hospitali ilikuwa inawapatia chakula tu kama ndugu zao wakishindwa kufanya hivyo.
Takribani wagonjwa kati ya 600 na 700 ambao rufaa zao ni kutoka Hospitali za Dar es Salaam walikuwa hawapati chakula kutoka Hospitalini, na ilibidi ndugu zao wawaletee chakula. Hata hivyo, Hospitali ilikuwa inawapatia chakula tu kama ndugu zao wakishindwa kufanya hivyo.
Hitimisho.
“Uongozi wa Hospitali unaamini kwamba
mabadiliko haya hayatamuongezea mgonjwa gharama, bali yatampunguzia gharama
pamoja na ile adha kama ilivyoainishwa hapo juu. Aidha, uongozi unaamini kwamba
uamuzi huu unaendana na azma nzima ya kuboresha utoaji huduma katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili na kuboresha mazingira ya Hospitali. Tunaomba ushirikiano
wenu katika kutekeleza jukumu hili ili kusudi wagonjwa waweze kuhudumiwa vizuri
zaidi” alisisitiza Bw. Aligaesha.
No comments:
Post a Comment