MKUU wa Majeshi nchini, Davis Mamunyange (pichani kushoto), ameliagiza jeshi la polisi na vikosi vya Usalama Tanga kuhakikisha majambazi waliofanya mauaji ya kutisha kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga wanakamatwa haraka.
Ameyasema hayo jana wakati wa mazishi ya watu 8 waliouwawa kwa kuchinjwa usiku wa Jumatatu na kusema kuwa msako wa kuwatafuta watu hao ufanyike mara moja.Amewahakikishia wananchi wa Amboni na Tanga kwa ujumla kuwa Jeshi la Wananchi na vyombo vyengine vya Usalama likiwemo Polisi kuwa tukio kama hilo haliwezi tena kujirudia.
Umati wa watu wa Kibatini, Amboni na Tanga
wakishiriki katika
mazishi ya watu 8
waliuwawa kwa
kuchinjwa na watu
wanaoaminika kuwa
ni majambazi
usiku wa Jumatatu.
|
Amesema kufuatia tukio hilo wananchi wameingiwa na hofu na kazi za kujiletea maendeleo kudorora ikiwemo kilimo na mifugo hivyo kuwataka kuongeza doria maradufu.
Usiku wa kuamkia juzi watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliwauwa watu 8 kwa kuwakusanya kwa pamoja na kuwachinja mmoja mmoja mbele ya uwanja wa nyumba ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji tukio ambalo limewashangaza watu wengi.
No comments:
Post a Comment