Na Rebeca Duwe,Tanga.
MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoa wa Tanga imewahukumu watu
wawili kwenda jela kifungo cha miaka 10 kutokana na kupatikana na hatia ya
kutumia nyaraka bandia benki ya NMB na kufanikiwa kuiba fedha.
Hukumu hiyo ya kesi namba 48 ya mwaka 2011 imetolewa juzi katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tanga,Aziza Lutala mbele ya wakili wa serikali,Rebeca Mwongoso akishirikiana na Regina Kayuni.

Waliohukumiwa kwenda jela ni Bakari
Mwalimu Jembe na Elias John Singano ambao wote wawili kwa pamoja wamekwenda
jela wakipewa kifungo cha miaka 10 kutokana na kupatikana na hatia ya kutenda kosa
hilo la kughushi na kuiba.Rebeca akishirikiana akiwasomea mashataka washitakiwa
hao alisema,washitakiwa hapo Aprili 15 mwaka 2011 walighushi hundi ya taasisi
ya mikopo ya FINCA iliyopo maeneo ya barabara 14 Jijini Tanga.
Alisema washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kughushi,kutoa nyaraka za uongo na kula njama na lile la wizi ambao walitengeneza hundi ya uongo ya Tsh 21 mil kupitia benki ya NMB Muheza.Aliendelea kusema kwamba fedha hizo zilitolewa kupitia benki ya NMB tawi la madaraka lililopo Jijini Tanga ambapo ziliweza kuingizwa kwenye Akaunti ya Elias John Singano yenye nambari 417250927.
Kwa mujibu wa mwanasheria huyo fedha hizo zilipitia akaunti hiyo zikidaiwa kutumika kwenda utengeneza kutengeneza Tshirt za FINCA jambo ambalo lilikuwa uongo huku fulana hizo zikitajwa idadi yake kuwa 2211 na thamani yake ikiwa Tsh 21 mil.
Mwanasheria huyo wa serikali alisema kuwa washtakiwa walikuwa wakielewa kwamba hakukuwa na tenda yoyote iliyotolewa na kwamba walikuwa wakijua kile ambacho walikifanya hadikufanikiwa kupewa fedha hizo.Ilielezwa mahakamani hapo kwamba baada ya Singano kuzitoa fedha hizo alimpatia Bakari Jembe ambaye naye alimgawia mtoaji ‘Singano’ kiasi cha Tsh 3 milioni.

No comments:
Post a Comment