Wabunge
wa majimbo ya Mkoa wa Tanga wameahidi kujenga nyumba nne kwa ajili ya makazi ya
kaya ambazo ndugu zao waliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana katika
kitongoji cha Kibatini, Jumanne ya wiki iliyopita.
Wakazi hao walihamia katika eneo la Kona Z baada ya ndugu zao wanane kuchinjwa na watu hao katika tukio linaloonekana kama kulipiza kisasi baada ya wakazi hao kuwaripoti polisi watoto wanane walioonekana kwenye kitongoji chao na kutiliwa shaka.
Wabunge
waliahidi kujenga nyumba hizo baada ya kukuta familia hizo zikiishi katika
mazingira magumu kwenye makazi yao mapya huku vyombo vyao vikihifadhiwa
uwanjani.Walitoa ahadi hiyo june 4 mwaka huu walipokwenda kutoa rambirambi kwa
familia hizo.
Wabunge
hao wote wakiwa wa CCM ni Adadi Rajabu wa Muheza, Jumaa Awesso na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
“Hii
haiwezekani, binadamu hawezi kuishi katika mazingira kama haya, hawa wananchi
wapo katika machungu ya kufiwa, inatia simanzi kuona wamehamia huku, lakini
hawana pa kuishi,”
alisema Ummy ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu.
Alisema
wabunge wa mkoa wa Tanga kupitia CCM watajenga nyumba nne Kona Z kwa ajili ya
familia hizo, wakiwamo ndugu watatu wa familia moja ya marehemu Issa Hussein
aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji.
Mbunge wa
Pangani Awesso kushoto,
Adadi Rajab wa
Muheza (kulia)
na katikati
Ummy Mwalimu wakiwa
katika nyumba
walikohifadhiwa wafiwa
na wahanga wa
tukio la mauaji
Jumatu usiku
wiki iliyipita.
|
“Tumekubaliana
kwamba ujenzi huu utaanza mara moja wiki ijayo na tunataka nyumba zikamilike
haraka ili wafiwa hawa waondokane na adha ya kukosa makazi,”
alisema Awesso ambaye ni Mbunge wa Pangani.
Awesso
aliitaka Serikali kuhakikisha inalinda maisha ya wakazi wa maeneo hayo pamoja
na kufanya uchunguzi utakaowezesha kuwanasa walioshiriki mauaji hayo.Wafiwa hao
waliwaomba wabunge kuvishinikiza vyombo vya ulinzi na usalama kuweka ulinzi
katika eneo hilo ili wasichinjwe watu wengine kwa kuwa bado wana hofu kwamba
wanaweza kufuatwa.
“Kama
mnavyoona tumekuja huku sisi kama tulivyo, tumeacha kila kitu Kibatini, mazao
mashambani na mifugo tumeamua kukimbia ili kuokoa maisha yetu kwa hivyo
tunakabiliwa na ukosefu wa chakula,” alisema Mwanaisha Hassan.
No comments:
Post a Comment