Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa
habari wa Chanel Ten mkoani hapa, Daudi Mwangosi(pichani), Pacificus Simoni ametoa
ushahidi wake mbele ya mahakama na kuieleza kuwa alilazimishwa kusaini ungamo
mbele ya mlinzi wa amani bila kujua nini kilichoandikwa.
Alidai
kuwa baada ya kutoka kuhojiwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) na Ofisa wa
Makosa ya Jinai ya Mkoa (RCO), akifananishwa na picha ya gazeti la Mwananchi la
Septemba 3, 2012 alipokana siyo yeye, alipelekwa kwenda kufanya ungamo kwa
mlinzi wa amani, Frola Mhelela ambaye alikuwa shahidi namba tatu.
Alidai
wakati anakwenda kwa mlinzi wa amani alisindikizwa na Staff Sajent Erick,
ambaye alikuwa ameshika bahasha na kumkabidhi kwa mlinzi huyo.
Mtuhumiwa
huyo alidai mlinzi huyo alitoa karatasi na kuisoma kisha baadaye alimuambia
aisaini, naye bila kuhoji alisaini ile karatasi kwa sababu ilitoka kwa kiongozi
wake ambaye ni RCO, Nyegesa Wankyo.
Katika
kesi hiyo wakili wa utetezi, Rwezaura Kaijage aliiomba Mahakama kwamba mawakili
wa upande wa Jamhuri wataleta majumuisho ya mwisho leo.
Hata
hivyo, upande wa jamhuri ambao uliongozwa na wakili Sunday Hyera, ulisema
hawana pingamizi lolote juu ya upande wa utetezi baada ya kukaa na kukubalina
kwa pande zote mbili saa nane mchana watawasilisha majumuisho hayo.
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Dk Paulo Kihwelo alisema Mahakama imekubali
ombi la wakili wa utetezi kuleta majumuisho, huku Juni 27 wakisikiliza maoni ya
wazee wa baraza kwa ajili ya kupanga hukumu.
No comments:
Post a Comment