CLOPP
AONGOZA MBIO ZA KUMSAINI SADIO MANE
Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp huenda akaizidi keta klabu
ya Man Utd katika mpango wa usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Senegal
pamoja na klabu ya Southampton, Sadio Mane.Klopp ameonyesha dhamira hiyo,
kufuatia kuafiki mpango wa usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka
24, ambao huenda ukamgharimu kiasi cha Pauni milioni 25.
Meneja huyo kutoka nchini
Ujerumani, ameonyesha kuwa na dhamira ya kweli katika mpango huo, tofauti na
ilivyo kwa Man Utd ambao mara kadhaa hawajihusishi sana na harakati za usajili
wa Mane.
Endapo Mane, ataondoka Southampton,
wakati wa majira ya kiangazi kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 25,
ataiwezesha klabu hiyo kujipatia faida ya Pauni milioni 13.
Miaka miwiwli iliyopita, The
Saint walimsajili mshambuliaji huyo kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 12,
akitokea nchini Uswiz alipokua akiitumikia klabu ya Salzburg.
Klopp alianza kuvutiwa na Mane,
tangu alipoonyesha kiwango cha hali ya juu wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka
nchini England msimu uliopita, kati ya Southampton dhidi ya Liverpool, ambao
ulimalizika kwa majogoo wa jiji kukubali kisago cha mabao matatu kwa mawili.
CHELSEA YAPANIA KUNASA SAINI YA BEKI YA
NAPOLI
KLABU ya Chelsea inadaiwa kuanza
kumuwania beki wa Napoli Kalidou Koulibaly kwa kutoa ofa ya paundi milioni
19.2. Chelsea wamekuwa wakimhusudu kwa kiasi kikubwa beki huyo wa kimataifa wa
Senegal, ambaye ameingia katika mzozo na klabu yake kuhusiana na uhamisho wake.
Hata
hivyo, ofa hiyo ya Chelsea tayari imeshakataliwa na Napoli wamedai wanataka
kitita cha paundi milioni 30 ili waweze kumuachia nyota huyo mwenye umri wa
miaka 24. Napoli walichukizwa na Koulibaly kufuatia madai aliyotoa kuwa yuko
tayari kuzungumza na Chelsea.
Beki
huyo amesema hajazungumza na Antonio Conte lakini anadhani hilo litafanyika
hivi karibuni.
NOLITO ANUKIA MAN CITY
KLABU ya Manchester City,
inadaiwa kukaribia kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Nolito
kutoka Celta Vigo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amethaminishwa kwa kiasi
cha euro milioni 18 katika mkataba wake, na rais wa Celta Vigo Carlos Mourino
tayari ameshadokeza kuwa anategemea ataondoka kiangazi hiki.
Taarifa
zilizotolewa na gazeti la Gurdian la Uingereza zimedai kuwa City wana uhakika wa
kukamilisha dili hilo na kuongeza kuwa Nolito tayari ameshakubali mambo binafsi
katika mkataba wa miaka mitatu atakaopewa wenye thamani ya euro milioni nne
kila msimu. Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona, ambaye amecheza katika mechi
zote tatu za Hispania katika michuano ya Ulaya inayoendelea nchini Ufaransa,
amekuwa pia akihusishwa na tetesi za kurejea Camp Nou.
Nolito
ambaye atafikisha miaka 30 Octoba mwaka huu, aliondoka Barcelona na kwenda
Benfica mwaka 2011 kabla ya kujiunga na Celta Vigo miaka miwili baadae.
MADRID
YATHIBITISHA KUMREJESHA MORATA.
KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa
Alvaro Morata atarejea Santiago Bernabeu kipindi hiki cha kiangazi. Taarifa
hizo zimekuwa mapema baada ya mkurugenzi mtendaji wa Juventus Beppe Marotta
kubainisha kuwa Morata anategemewa kurejea Madrid.
Madrid
walikuwa na nafasi ya upendeleo ya kumnunua tena Morata mwenye umri wa miaka
23, ikiwa ni sehemu ya mkataba uliopelekea nyota huyo wa kimataifa wa Hispania
kujiunga na Juventus miaka miwili iliyopita na sasa wamethibitisha kufanya
hivyo.
Katika
taarifa yao iliyotumwa katika mtandao, Madrid walithibitisha taarifa hiyo na
kudai kuwa Morata atajiunga na mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa La Liga
chini ya meneja Zinedine Zidane. Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa Madrid
wanaweza kumuuza Morata kwa klabu nyingine ili wapatefaida.



No comments:
Post a Comment