MGOGORO WAZIDI KUITAFUNA AFRICAN SPORT YA TANGA
Wakizungumza katika kikao kilichofanyika katika Club hiyo wamesema kwasasa hawautambui uongozi ambao upo kwani ndio chanzo cha timu hiyo kushuka daraja.
Hata hivyo Wanachama hao wanashindwa kufahamu kwakuwa kumebaki mwezi mmoja kwa msimu mpya Ligi bila kuona Club inafanya usajili kwa wachezaji inaonyesha nieazi viongozi wamekosa mapenzi na club hiyo .
Aidha Mwenyekiti wa mkutano huo Isilam Abdala pamoja na Mohamedi Kidege wamesema hawata kubaliana na Mtu moja ndani ya Club kuwa na nafasi 5 yeye mtu mmoja.Mmmoja wa viongozi hao Katibu Ezi ndiye anayedaiwa kuwa na nafasi 5 ndani ya club hiyo.
YANGA YAMWITA KESSY MAANDALIZI YA MICHUANO YA CAF.
Rasmi
kesho Jumanne, beki mpya wa timu ya Yanga, Hassan Kessy ataanza kufanya mazoezi
na timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kwanza wa makundi wa Kombe la
Shrikisho Afrika.Yanga itaanza kampeni zake za makundi kwa kuvaana na Mo Bejaia
ya Algeria mchezo unaotarajiwa kupigwa Juni 17, mwaka huu.
Kessy
ambaye ametua Yanga hivi karibuni na kupewa mkataba wa miaka miwili akitokea
Simba, ataungana na wachezaji wengine wa klabu hiyo inayonolewa na Mholanzi,
Hans van Pluijm, baada ya kupewa mapumziko ya takribani wiki moja na nusu.Meneja
wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema kambi hiyo itaanza rasmi Jumanne huku wachezaji
wote waliopo nchini na nje ya nchi wakitarajia kuanza kuingia leo Jumatatu
kabla ya kuanza kwa maandalizi yao hayo.
“Rasmi
tunaanza kambi yetu Jumanne (kesho), kwa ajili ya kuanza kujiandaa na michezo
ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, kambi hiyo itaanzia hapahapa Dar na
wachezaji wataanza kuwasili kesho (leo) Jumatatu kwa wale wa ndani na nje ya
nchi.
“Wachezaji
wetu wote wapya ikiwemo Hassan Kessy naye pia anatarajia kuwa miongoni mwa hao
kwa sababu ni mchezaji wetu na tumemsajili tayari, hivyo ni lazima awepo katika
kambi yetu hiyo,” alisema Hafidh.
Yanga
imepangwa Kundi A, pamoja na timu za MO Bejaia ya Algeria, Medeama (Ghana) na
TP Mazembe (DR Congo).
No comments:
Post a Comment