uchafu ukiwa umetupwa hovyo kwenye eneo lisilo
rasmi ambalo wakazi wa mitaa ya chumbageni na kwaminchi wanalitumia kama dampo
ambalo sio rasmi.
|
Wakazi wa Mtaa
wa Chumbageni Jijini Tanga wameitaka Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mjini
Tanga (TANGA-UWASA) kutatua kero ya kuziba kwa mfereji wa maji taka
unaotiririsha maji machafu kwenye makazi ya watu.
Mchuuzi wa Samaki
Soko la Deep Sea
|
Wakizungumza
na mwandishi wetu hapo jana Wakazi hao wamesema mfereji huo umeziba kwa zaidi
ya wiki moja sasa na tayari wamewasiliana na Mamlaka hiyo ili kutafuta ufumbuzi
wake lakini mpaka sasa bado haijafanyiwa kazi na maji machafu hayo yanaendelea
kutiririka kuelekea kwenye soko la Samaki la Deep Sea jambo linaloweza
kusababisha magonjwa ya milipuko kwa wakaazi wa maeneo hayo.
Mmoja wa wakaazi hao Sistr Makrina Petro
amesema harufu kali inayotokana na maji hayo imekuwa kero na amezitaka mamlaka
husika iwajibike haraka kuondoa kero hiyo.
Akizungumza na kituo hiki M/Kiti wa Serikali
ya Mtaa huo Bi Asha Ziggiy amesema kukosekana kwa dampo la kutupa taka kwenye
mtaa huo kunapelekea baadhi ya wakazi wake kutupa taka kwenye mifereji na
kupelekea kuziba na kushindwa kupitisha maji taka.
No comments:
Post a Comment