Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa tamko
zito kikitaka Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika mwezi ujao,
vinginevyo watatumia nguvu ya umma kuuzuia.
CCM kimeitisha mkutano mkuu maalumu
unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mjini Dodoma, kwa lengo la Mwenyekiti wa chama
hicho, Jakaya Kikwete kumkabidhi uongozi wa chama, Rais John Magufuli.
Kauli ya kutaka Polisi kuzuia
mkutano huo kama inavyofanya kwa vyama vingine vya siasa, ilitolewa juzi mjini
Moshi na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Julius Mwita.
Msimamo huo wa Chadema ambao
uliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalim
unafuatia Polisi kuzuia mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni wanachama
wao.
Akizungumza na wanahabari, Mwita
alikwenda mbali na kudai kuwa, Chadema watalifungulia Jeshi la Polisi kesi ya
madai ya fidia kwa kuvuruga mahafali ya Chaso mjini Dodoma mwishoni mwa wiki
iliyopita.
“Ukisoma barua yao wamesema wamezuia
mikutano ya hadhara sasa kama wanakuja hadi kwenye vikao vya ndani, hatuwezi
kuendelea kukubali jambo hili.Tumetumia busara sana,” alisema Mwita na kuongeza:
“Msipouzuia Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma Julai 23 tunakuja kuuzuia sisi... yaani muwe tayari kusafiri kwenda Dodoma tukauzuie ule mkutano la sivyo, wauzuie kama walivyouzuia mikutano yetu.”
Mwita alimgeukia Mwalimu na kumweleza kuwa hiyo ni lugha ya ujana na inatekelezeka, akawahoji vijana wa Chaso waliokuwapo: “Wangapi mko tayari kuja Dodoma?” Wote wakaafiki.

“Intelijensia ya polisi ni ya
kiumbea, inayoweza kujua tu Chadema wanakwenda kwenye mkutano, haiwezi kujua
watu wamejificha wana bunduki na risasi 300 kwenye mawe kule Mwanza,” alidai.
Mwalimu alisema utaratibu wa Polisi
na Serikali lazima ukome na kwamba wao ni viongozi.
No comments:
Post a Comment